-
Rais wa Kenya atoa hotuba kali UNGA, asema mabadiliko ya Baraza la Usalama si 'kuifanyia fadhila Afrika'
Sep 25, 2025 03:11Rais wa Kenya William Ruto ametoa hotuba kali katika kikao cha 80 cha Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York siku ya Jumatano.
-
Tume ya uchaguzi Malawi yamtangaza Mutharika mshindi rasmi wa uchaguzi wa urais
Sep 25, 2025 03:11Tume ya Uchaguzi ya Malawi imemtangaza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika wa chama cha Democratic Progressive Party (DPP) mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16.
-
Umoja wa Afrika na nchi za Sahel kurekebisha uhusiano
Sep 25, 2025 01:01Mawaziri wa mambo ya nje wa Mali, Niger, na Burkina Faso wamefanya mazungumzo na Umoja wa Afrika kuhusu kurejesha ushirikiano, ikiwemo juhudi za pamoja za kupambana na ugaidi katika nchi zao.
-
Rais wa Malawi akubali kushindwa uchaguzi wa rais hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa
Sep 24, 2025 10:38Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo, akimtaja rais wa zamani Peter Mutharika kuwa "mshindi mtarajiwa".
-
Afrika Kusini yaitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki iamue kuwa Israel inatekeleza mauaji ya kimbari Gaza
Sep 24, 2025 08:25Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutoa uamuzi rasmi kuwa mauaji ya kimbari yanatekelezwa katika Ukanda wa Gaza, na kuamuru kusitishwa mara moja kwa machafuko hayo, kwa mujibu wa kauli ya Rais wa taifa hilo mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.
-
Mapigano ya kijeshi yashadidi kati ya SAF na RSF magharibi mwa Sudan
Sep 24, 2025 02:27Mapigano ya kijeshi yameongezeka katika siku za hivi karibuni kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Mutharika aongoza kwa kishindo katika kinyang’anyiro cha urais nchini Malawi
Sep 23, 2025 22:44Rais wa zamani wa Malawi, Peter Mutharika, ameibuka na uongozi wa kishindo katika hesabu za kura za uchaguzi wa urais, akijikusanyia takriban asilimia 66 ya kura zilizohesabiwa hadi sasa.
-
Tshisekedi: DRC haitapiga mnada rasilimali zake kwa Marekani
Sep 23, 2025 22:43Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, ametangaza kuwa licha ya msaada wa Marekani katika upatanisho wa migogoro, nchi yake haitauza kwa bei rahisi au kupiga mnada rasilimali zake kwa taifa hilo la Magharibi.
-
Rais wa Afrika Kusini atoa mwito wa kuwepo taifa huru la Palestina
Sep 23, 2025 08:25Wakati vita vya Israel dhidi ya Gaza vikiendelea, Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuhusu dhamira ya nchi yake ya kupatikana njia ya ufumbuzi wa mataifa mawili ili kuhitimisha mzozo uliodumu kwa muda mrefu kati ya Israel na Palestina.
-
Burkina Faso, Mali na Niger zatangaza kujiondoa ICC
Sep 23, 2025 08:25Mataifa ya Afrika Magharibi ya Burkina Faso, Mali na Niger yametangaza kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na kusema mahakama hiyo ni chombo cha ubeberu cha "Ukoloni Mamboleo".