Mehdi Safari: Iran inaweza kuimarisha uhusiano wake na BRICS licha ya vikwazo
(last modified Tue, 08 Aug 2023 15:11:32 GMT )
Aug 08, 2023 15:11 UTC
  • Mehdi Safari: Iran inaweza kuimarisha uhusiano wake na BRICS licha ya vikwazo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya uchumi amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaweza kuanzisha uhusiano na kundi la BRICS linaloundwa na nchi zinazoibukia kiuchumi, licha ya kukabiliwa na vikwazo haramu vya Marekani.

Mehdi Safari ameeleza haya akihutubia mkukano ulifanyika kwa anwani: "Iran na BRICS: Matarajio kwa Ajili ya Ushirika na Ushirikiano." Mkutano huo umefanyika leo katika Taasisi ya Masuala Mafunzo ya Kisiasa na Kimataifa ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, mjini Tehran. 

Safari ameongeza kuwa, licha ya vikwazo vya kikatili vya upande mmoja, Iran ina uwezo mzuri wa kuendeleza uhusiano na BRICS. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelitaja kundi la BRICS linaloundwa na mataifa matano kama mojawapo ya washirika wakuu wa Tehran.

Kundi la BRICS 

Wakati huo huo Mehdi Safari amezipongeza nchi wanachama wa BRICS kwa uwezo wao uliozipelekea kuanzisha taasisi muhimu kama hii miongoni mwa jamii ya kimataifa. 

Kundi la BRICS linaundwa na nchi zinazoibukia kiuchumi ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika kusini. Kundi hili  limekuwa likitazamwa kama mbadala wa kambi ya Magharibi ya kuhodhi uchumi na siasa za ulimwengu.