Oct 24, 2023 07:26 UTC
  • Ebrahim Raisi: Bilikuli utawala wa Kizayuni hauwezi kuwa rafiki wa nchi yoyote ya Kiiislamu

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katu utawala wa Kizayuni wa Israel hauwezi kuwa rafiki wa nchi yoyote ya Kiiislamu.

Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Jeyhun Bayramov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Azerbaijan aliyeko hapa nchini kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa 3+3 wa kundi la ushirikiano wa Caucasia na kubainisha kwamba, Iran inaamini kuwa, njia bora kabisa ya kupatia ufumbuzi matatizo na mizozo katika eneo hili ni mazungumzo baina ya mataifa ya eneo.

Katika mkutano huo, Ebrahim Rais amegusia msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, matatizo ya eneo hili hayawezi kutatuliwa kwa kuingilia kati vikosi vya kigeni, na kusisitiza kwamba,  suluhisho la matatizo ya kikanda linawezekana kupitia ushirikiano mkubwa miongoni mwa nchi za eneo.

Rais Ebrahim Raisi akimkaribisha Jeyhun Bayramov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Azerbaijan

 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kwa kusema kuwa, huko nyuma nimewahi kumwambia Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel hauwezi rafiki yako au rafiki wa nchi yoyote ya Kiislamu.

Kadhalika Rais Ebrahim Raisi ameeleza kuwa, hali ya mambo inayoshuhudiwa hii leo huko Gaza ni ushahidi tosha kwa nchi zote za eneo kuona kwamba, Wamagharibi wakiongozwa na Marekani, kupitia misaada yao kamili kwa jinai za Wazayuni, ni jinsi gani wanathibitisha kwamba sio tu marafiki na waungaji mkono wa nchi za eneo hili, bali wanachokifuatilia ni kufikia maslahi yao ya kibaguzi katika eneo la Asia Magharibi.

Tags