Jun 17, 2024 12:53 UTC
  • Ali Akbari: Ushiriki mkubwa zaidi katika uchaguzi huongeza mshikamano na nguvu ya taifa

Khatibu wa Sala ya Eidul Adh'ha mjini Tehran amesema kuwa, ushiriki mkubwa zaidi katika uchaguzi kutaongeza mshikamano na nguvu ya itaifa

Hujjatul-Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema hayo katika hotuba za Swala ya Edul Adh'ha iliyosaliiwa leo hapa mjini Tehran ambapo sambamba na kuelezea umuhimu wa uchaguzi ujao wa Rais hapa Iran amesema kuwa, Rais ajaye wa taifa hili anapaswa kuwa na azzma, irada na tadibiri imara kama shahidi Ebrahiim Raisi.

Kadhalika ameeleza kwamba, sifa muhimuu ya Rais ajaye ambayo anapaswa kuwa nayo ni kuwa mwaminifu, mwenye kufungamana na fikra na njia ya Imam KKhomeini  na mwenye kuchunga na kuheshimu haki za jamii ya Kiislamu na mwenye kutunza amana. Sheikh Akbari amezungumzia umuhimu wa sikukuu ya Eidul Adh'ha na mtihani aliopewa Nabii Ibrahim (as) pale alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu amchinje mwanawe Ismail (as) na kueleza kwamba, Nabii Ibrahim alifaulu mtihani huu katika siku kama ya leo.

Khatibu wa Sala ya Eidul Haj mjini Tehran amezungumzia pia umuhimu wa kusalimu amri mbele ya amri na maagizo ya Mwenyezi Mungu na kuashiria jinsi Nabii Ebrahim na mwanawe Islamil walivyosaliimu amrii mbele ya amri ya Mwenyezi Mungu na hivyo kupandishwa daraja kwa hatua yao hiyo.