Iran yatengeneza dawa ya vidonda vya mguuni vinavyosababishwa na kisukari
(last modified Mon, 11 Nov 2024 07:58:08 GMT )
Nov 11, 2024 07:58 UTC
  • Iran yatengeneza dawa ya vidonda vya mguuni vinavyosababishwa na kisukari

Kwa mara ya kwanza, kampuni ya maarifa ya kisayansi na ujuzi ya Iran imefanikiwa kusambaza dawa ya kutibu vidonda vya miguu vinavyosababishwa na maradhi ya kisukari na vile vya kuungua.

Wagonjwa wa kisukari hupata majeraha makubwa hasa sehemu za miguuni; na kwa bahati mbaya kutochukuliwa tahadhari na kupata matibabu kwa wakati hupelekea mgonjwa kukatwa kiungo; hivyo matibabu ya uhakika ya majeraha ya miguu kwa wagonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa. 

Mtandao wa Sahab umemnukuu Fahima Muhammad Hosseini Mkuu wa Masuala ya  Sayansi, Teknolojia na Msingi wa Maarifa katika Ofisi ya Rais,  ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Danesh Bunyan ya Iran na kuripoti kuwa: 'Kwa mara ya kwanza nchini Iran, kumetengenezwa dawa kwa jina la "Bernamine". Dawa hii inatumika kutibu vidonda vya miguu vya wagonjwa wa kisukari na vidonda vya daraja la 3 na 4 vya watu walioungua moto.

Bi Muhammad Hosseini ameongeza kuwa, dawa hiyo hutumika kuponya jeraha na kuotesha tishu.