Jeshi la Wanamaji la IRGC: Tutatoa jibu kali kwa tishio lolote
-
Brigedia Jenerali Tangsiri
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kikosi hiki, kinategemea uwezo wa kielimu wa wataalamu wa ndani, na leo hii kina uwezo wa kutoa jibu madhubuti na kali kwa tishio lolote."
Akigusia nafasi ya kikosi hiki katika kuhakikisha usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia, Kamanda wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Alireza Tangsiri, amesisitiza kuwa: "Leo hatutegemei tena nguvu yoyote ya kigeni, na Jeshi la Wanamaji la IRGC linapiga hatua za maendeleo kwa kutegemea makampuni ya ndani yanayotegemea ujuzi na maarifa."
Brigedia Jenerali Tangsiri ameendelea kusema: "Ghuba ya Uajemi ni ya Iran na itabaki kuwa ya Iran, na tunawajibika kuilinda Ghuba ya Uajemi yenye urefu wa kilomita 1,375 na upana wa kilomita 380, yenye eneo la kilomita za mraba 250,000."
Akizungumzia misaada ya Wamarekani kwa utawala wa dikteta wa zamani wa Iraq katika kushambulia visima vya mafuta vya Iran katika Ghuba ya Uajemi, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la IRGC amesema: "Jeshi letu pendwa la Wanamaji, kwa shida kubwa, juhudi zisizosita na kujitolea kwa makumi ya mashahidi, liliweza kudumisha mtiririko wa mafuta nje ya nchi."
Akizungumzia uwezo wa Jeshi la Manawaji la Iran, Brigedia Jenerali Alireza Tangsiri amesema: "Wakati Green Beret wa Uingereza walipoingia kwenye maji ya nchi yetu walidhani wanaweza kuzunguka katika eneo hili kama zamani; tuliwakamata na kuwapigisha magoti ili waelewe nguvu ya watoto wa nchi hii."
Amesisitiza kuwa: "Iwapo watashambulia na kukamata vyombo na meli zetu popote duniani, sisi pia tutakamata vyombo vyao kama tulivyofanya hadi sasa.