Rouhani: Uzalishaji gesi kuongezeka kufikia mwishoni wa mwaka huu
Rais wa Iran amesisitiza kutumiwa mazingira yaliyojitokeza baada ya makubaliano ya JCPOA kwa ajili ya kustafidi na teknolojia mpya na kueleza kuwa uzalishaji wa gesi nchini Iran utaongezeka kwa mita mraba milioni 140 kwa siku hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Hujjatul Islam wal Muslimin Hassan Rouhani amesema leo hapa Tehran katika sherehe za kuadhimishwa mwaka kwa 50 tangu kuasisiwa Shirika la Taifa la Gesi la Iran kuwa, awamu za 18,19, 20 na 21 za Pars Kusini zitaingia kwenye mzunguko, na kwamba wanataraji kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu uzalishaji wa gesi kwa siku utaongezeka kwa karibu mita mraba milioni 140.
Rais Rouhani amebainisha kuwa suala la mafuta na gesi siku zote limekuwa na nafasi muhimu kwa wananchi; na kuongeza kuwa mafuta na gesi si kwa ajili tu ya masuala ya kiuchumi, na kwamba tangu kuanza kuzalishwa kwake nchini Iran uzalishaji huo umekuwa ukiambatana na masuala ya kisiasa kwa muda mrefu.