Watu karibu milioni 55 wametimiza masharti ya kupiga kura nchini Iran
(last modified Mon, 15 Feb 2016 03:07:26 GMT )
Feb 15, 2016 03:07 UTC
  • Watu karibu milioni 55 wametimiza masharti ya kupiga kura nchini Iran

Mohammad Hussein Muqimi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Iran ametangaza kuwa, raia milioni 54, laki tisa na elfu kumi na tano na ishirini na nne wametimisha masharti ya kupiga kura katika uchaguzi ujao wa mwezi huu wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Bwana Muqimi amesisitiza mbele ya waandishi wa habari kwamba, tume yao imeandaa vituo 31 vikuu na vingine 1031 vidogo vidogo kwa ajili ya uchaguzi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Aidha amebainisha kwamba, kwa ajili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, tume hiyo imetayarisha vituo vikuu 207 na vingine 855 vidogo vidogo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Iran ameongeza kuwa, idadi ya masanduku itaainishwa baada ya kamati za utendaji kupasisha suala hilo.

Chaguzi za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa pamoja zimepangwa kufanyika tarehe 26 ya mwezi huu wa Februari.

Tags