Qalibaf amwambia Trump: Kutii maagizo ya Netanyahu kutawasha moto kwenye kanda nzima
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137822-qalibaf_amwambia_trump_kutii_maagizo_ya_netanyahu_kutawasha_moto_kwenye_kanda_nzima
Spika wa Bunge la Iran amejibu vitisho vya hivi karibuni vya Donald Trump, rais gaidi wa Marekani katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema tabia yake ya kutii na kufuata maagizo ya waziri mkuu katili wa Israel Benjamin Netanyahu kutawasha zaidi moto wa vita katika kanda nzima ya Magharibi mwa Asia.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Apr 06, 2026 02:28 UTC
  • Mohammad Baqer Qalibaf
    Mohammad Baqer Qalibaf

Spika wa Bunge la Iran amejibu vitisho vya hivi karibuni vya Donald Trump, rais gaidi wa Marekani katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema tabia yake ya kutii na kufuata maagizo ya waziri mkuu katili wa Israel Benjamin Netanyahu kutawasha zaidi moto wa vita katika kanda nzima ya Magharibi mwa Asia.

Mohammad Baqer Qalibaf amesema katika ujumbe huo kwamba: "Kung'ang'ana kwako kutii maagizo ya Netanyahu kunawasha moto eneo zima la Magharibi mwa Asia. Hatua zako zisizo na msingi zitaigeuza Marekani kuwa jahanamu halisi kwa kila familia ya Marekani."

Katika taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Mehr, Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran ameongeza kwamba: Acha kufanya makosa; kwa uhalifu wa kivita hutapata mafanikio yoyote. Njia pekee ya kweli ni kuheshimu haki za taifa la Iran na kukomesha mchezo huu hatari.

Spika Qalibaf ametuma ujumbe huo akijibu matusi na vitisho vya Rais wa Marekani, Donald Trump aliyesema, kama Iran haitakubali kuketi kwenye meza ya mazungumzo na Washington ataanza kuangamiza madaraja na miundombinu ya kiraia nchini Iran.

Matamshi hayo yamelaaniwa kimataifa yakitajwa kuwa ni kielelezo cha uhalifu wa kivita unaopaswa kufuatiliwa katika mahakama husika.