Wamarekani wanapaswa kujua kwamba wakati hautarudi nyuma
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu- Siku ya Arafa
Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuwadia msimu wa Hijja ya Nabii Ibrahim (as), Ayatullah Seyyed Mojtaba Hosseini Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametaja amali na thikri zilizajaa maana za Hijja na kusema ni ishara za kudumu milele kwa wanadamu kwa ajili ya kuwahamasisha waelekee kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuwa huru kutokana na minyororo ya Shetani na wafuasi wake, na wakati huo huo kufanya bidii bila kuchoka kwa ajili ya kuondokana na matamanio ya nafsi, na kufikia sa
Ameashiria suala la taifa kubwa la Iran kuegemea kwenye ishara hizo hususan silaha ya “Allahu Akbar” tangu zama za harakati na hatimaye ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na vile vile zama za Vita vya Kujitetea Kutakatifu hadi Vita vya Pili na vya Tatu vya Kulazimishwa, na kushindwa adui kuilazimisha Iran ijisalimishe, na tukio la kimiujiza la kubaathiwa wananchi na kusisitiza: Mwaka huu, suala la kujibari na kujitenga mushirikina lina umuhimu maradufu, na kina na upeo wa kujitenga na Marekani na utawala wa Kizayuni unavuka mipaka ya ibada ya kujibari na maadui katika msimu wa Hijja, na kwamba kuanzia sasa, "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel" zitakuwa nara za pamoja za Umma wa Kiislamu na wanaodhulumiwa duniani na hasa vijana.
Ujumbe kamili wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Umma wa Kiislamu uliosomwa Jumanne asubuhi na Hujjatul Islam Walmuslimin Nawwab, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu na Msimamizi wa Mahujaji wa Iran katika Jangwa la Arafat ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
لبَّیک اللّهمّ لبَّیک، لبَّیک لا شریک لک لبَّیک، إنّ الحمد و النّعمة لک و المُلک
Ewe Mwenyezi Mungu! Naitikia wito Wako, huna mshirika, na sifa zote nzuri, neema zote, na ufalme na nguvu zote zinatoka Kwako na ni Zako.
Msimu wa Hija wa mwaka huu umewadia, na mahujaji wa Umma wa Kiislamu wameingia katika hali ya utumwa na kusoma Talbiyah ili kuhama kutoka maisha ya kimaada na ya kawaida kwenda kwenye maisha ya kimungu na ya saada; maisha ya Tauhidi yaliyojikita katika utumwa na ucha-Mungu, na kufukuza, kukanusha, na kutomshirikisha Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, fursa ya kuhama huku si ya mahujaji wanaohiji mwaka huu tu katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu, bali pia ni ya ndugu na dada Waislamu wote nchini Iran na duniani kote, kuanzia wale waliohiji katika miaka ya nyuma ya maisha yao hadi wale ambao bado hawajafaulu kuhiji.
Sharti la kuhama huku ni kuvaa ihramu ya kudumu ya kumdhikiri Allah; ni tawafu na mzunguko wa kudumu kwenye mhimili wa haki; ni Sai' na kwenda na kurudi daima katikati ya vilele nyeti vya majukumu ya kimungu; ni ramy na kurusha mawe daima dhidi ya Shetani mwovu, pamoja na madhihirisho yake yote ya kuvutia na wafuasi na hila zake zote; ni Wuquf na kisimamo kilochochanganyika na mazingatio na unyenyekevu katika dua; ni kuwalisha masikini waliokamwa na wapita njia, ni kutoa mhanga matamanio yanayopotosha na kuondoa uchafu wa ndani. Na katika hali zote, ni kuwa tayari kutumikia na kuinua bendera ya kutetea haki.
Na hivi ndivyo lilivyokuwa taifa la Iran katika Miqaat na eneo la Mapinduzi ya Kiislamu ambapo lilipiga hatua katika njia hii hii ya hijra na kuhama, likaitikia wito wa Nabii Ibrahimi kupitia Khomeini Mkubwa, likavua vazi la kunyenyekea, na kuvaa ihramu ya saada ya dunia na akhera, na kwa kuitikia na kufanya sai, likafanya juhudi za kuuzunguka mhimili wa mafundisho ya Uislamu ulio safi na wa Mtume Muhammad (saw), na hivyo kujikurubisha na nuru ya uadilifu wa ulimwengu wote, na fakihi mkuu mtawala. Allahu Akbar, Allahu Akbar, La ilaha illallahu, wa Allahu Akbar, Allahu Akbar, wa Lillahil Hamd, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Ala Ma Hadana.
Nam, Allahu Akbar; na ni kwa silaha hii ya Mwenyezi Mungu ni Mkubwa ndipo taifa la Kiislamu la Iran lilianzisha mapambano yake miaka 47 iliyopita, na kuupindua utawala dhalimu, wa kidikteta, na tegemezi wa Pahlavi, na kuikata mikono na miguu ya Marekani yenye pupa na kiburi kutoka nchini humu, na kukata kabisa upenyaji wa Uzayuni.
Ni kwa silaha hii hii ya Allahu Akbar ndipo, baada ya uvamizi wa utawala wa Baath wa Saddam katika ardhi ya Iran, Mujahidina shupavu na vijana waliojitolea mhanga wakaanzisha Kujitetea Kutakatifu kwa miaka 8 na, licha ya uungaji mkono na nguvu zote za Mashariki na Magharibi kwa utawala wa Baath, lakini waliweza kumshinda na kumketisha sehemu aliyostahili. Mapambano na muqawama huu uliendelea miaka mingi baadaye mbele ya mzigiro wa kiuchumi, majaribio ya mapinduzi, vikwazo vya kidhalimu, mashambulio yasiyohesabika ya kisiasa, kipropaganda na kiuchumi ya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Allahu Akbar; ni silaha hii ya Allahu Akbar ndiyo iliyoimarisha uhusiano kati ya Umma wa Kiislamu na vijana Mujahidina wa mrengo wa Muqawama kutoka Iran hadi Lebanon, Palestina, Iraq na Syria, kutoka Afrika na Yemen hadi Afghanistan na Pakistan, na mataifa yote huru ya dunia, ili kuwawezesha kusimama na kushikamana na kamba hii madhubuti katika kutetea Ummah wa Kiislamu dhidi ya wavamizi maghasibu wa Kizayuni, kuondoa uvimbe wa Daesh, kuanzisha operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa na hivyo kubana pumzi za utawala unaoyumba wa Kizayuni.
Allahu Akbar; Nam, Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni Mkubwa zaidi kuliko maelezo. Silaha hii ya Allahu Akbar ndiyo ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliitumia na kufanikiwa kutoa vipogo vikali dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Vita vya Pili vya Kulazimishwa vya Khordad 1404 (sawa na Juni 2025), kutoa pigo kubwa kwa Marekani mvamizi, na hivyo kumzuia adui kufikia lengo lake la kuitaka Iran eti ijisalimishe.
Na silaha ya Allahu Akbar ililipa nguvu na uwezo mkubwa taifa la Iran kiasi kwamba baada ya tukio la kusikitisha na kuhuzunisha la kuuawa shahidi Kiongozi Muadhamu, mtoto na mrithi wa Mtukufu Mtume Mtukufu (saw), Ayatullah Seyyed Ali Hosseini Khamenei, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliyeuawa na watu waovu zaidi katika dunia ya leo, taifa la Iran likabaathiwa ambapo kwa uwepo wake wa pande zote katika kila uwanja lilipohitajika, likawashangaza walimwengu kwa ujasiri na fahari yake.
Ni kweli kabisa kwamba, Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko maelezo. Ni kwa silaha hii ya Allah Akbar ndipo wapiganaji shupavu na vikosi vya kijeshi vilivyojitolea muhanga katika Iran ya Kiislamu, wakishirikiana na Mujahidina wa Mrengo wa Muqawama, hususan katika nchi tukufu ya Lebanon, wakapata ushindi wa ajabu dhidi ya majeshi hayo mawili ya kigaidi na yaliyojizatiti vilivyo kwa silaha nzito, ya Marekani na utawala wa Kizayuni katika Vita vya Tatu vya Kulazimishwa. Kwa kumtegemea Mola Muumba na makombora pamoja na ndege zao zisizo na rubani ardhini, angani na baharini, walimshambulia vikali shetani mkubwa, yaani Marekani na mnyama wake aliyefunzwa, utawala wa Kizayuni, na hivyo kushuhudia kwa macho yao wenyewe ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu ya ushindi kwa Mujahidina katika njia ya Mwenyezi Mungu, ikitimia.
Allahu Akbar tena; Bila shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni Mkubwa kuliko chochote kinachoweza kuelezwa, na askari Wake ni bora kuliko uwezo wowote. Na ni kwa silaha hii ya Allahu Akbar ndipo kufuatia kubaathiwa taifa la Iran na mrengo wa Muqawama, kubaathiwa kwa Umma wa Kiislamu pia kutatimia, na hivyo kueneza kujibari na washirikiana kupitia ramy na kurusha mawe kwenye Hija, katika uwanja wa maisha ya mtu binafsi, kijamii na kisiasa ya Waislamu katika pembe zote za dunia. Umma wa Kiislamu na mataifa ya eneo yana uwezo na maslahi mengi ya pamoja ambayo yataunda mfumo mpya na dira ya baadaye ya eneo na dunia nzima.
Hapa, ninazitolewa wito wa dhati na ikhlasi nchi na serikali zote za Kiislamu kukumbutia urafiki na ushirikiano katika heri, ili tushirikiane na kuendeleza Umma wa Kiislamu na kutatua matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Lililo wazi katika uwanja huu ni kwamba masaa hayarudi nyuma, na mataifa na ardhi za eneo hazitakuwa tena makao ya kambi za Marekani. Marekani mbali na kuwa haitakuwa tena na kimbilio salama kwa maovu na uanzishwaji wa kambi za kijeshi katika eneo, inaendelea kupoteza hadhi yake ya zamani siku baada ya siku. Utawala unaolegalega wa Kizayuni na wenye uvimbe wa saratani pia unakaribia hatua za mwisho za maisha yake ya kuchukiza, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa mujibu wa maneno madhubuti na ya kuona mbali aliyoyatoa Kiongozi Muadhamu Shahidi miaka 10 iliyopita, Mwenyezi Mungu Amrehemu, miaka 25 baada ya hapo, utawala huo hautaiona tena historia.
Kwa ajili hiyo, mwaka huu suala la kujibari na washirikina lina umuhimu maradufu, na kina na upeo wa kujitenga na Marekani na utawala wa Kizayuni utavuka mipaka ya ibada ya kujibari katika msimu na wakati wa Hija, ambapo katika maeneo tofauti ya Iran na duniani baada ya siku hizi tukufu, nara ya mauti kwa Marekani na mauti kwa Israel itakuwa kauli mbiu ya pamoja ya Umma wa Kiislamu na wanyonge wa dunia nzima hususan vijana.
Mustakabali ni wa Umma wa Kiislamu na ustaarabu mpya wa Kiislamu, na kila mmoja wetu anaweza kuwa na nafasi katika kufikiwa mustakbali huu na kuukaribia zaidi kwa mujibu wa juhudi, uwezo na wajibu wa kila mmoja wetu. Mahujaji wa Iran na wa maeneo mengine wana nafasi nzuri na mahimu katika kusimulia kisa cha ushindi wa vita vya tatu vya kulazimishwa kwa ndugu na dada zao wengine Waislamu na kuwapa matumaini ya mustakabali mzuri.
Nawaomba mahujaji wote wapendwa muombee kuharakishwa kurejea kwa Mwokozi wa wanaadamu, Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake, umoja wa Umma wa Kiislamu, ukombozi wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa, kuondolewa matatizo makubwa ya Waislamu, na kufikiwa ushindi wa mwisho dhidi ya uistikari wa dunia, na pia nakukuombeni msisahau kunijumuisha kwenye dua zenu.
Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu na kumtumia salamu Muhammad na Aali Muhammad, na uwarehemu Mahujaji na Umma wote wa Kiislamu. Watakabalie Hija zao, ziangazie nyoyo zao kwa nuru za elimu na maarifa, na uimarishe azimio na nia yao ya kusonga mbele kwenye njia ya kuurekebisha Ummah na kupata ushindi wa mwisho dhidi ya maadui wa Uislamu.
Ewe Mwenyezi Mungu! Ziteremshie neema na rehema zako kubwa roho safi za mashahidi wa njia ya Mwenyezi Mungu, haswa mashahidi wa mrengo wa Muqawama, wakiongozwa na, Kiongozi Muadhamu Shahidi, Mwenyezi Mungu ainue hadhi yake, na waongoze Mahujaji, wafanya-ibada na wanaofanya juhudi waliojumuishwa katika miongozo ya Kiongozi wa Umma. Liongoze taifa la Iran na Umma wa Kiislamu katika kuendeleza njia na lengo lake.
Ewe Mwenyezi Mungu, mteremshie baraka na salamu zako bora zaidi Imam Mahdi-al-Mundhar, salamu na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu ya wazazi wake watoharifu. Na tujumuishe sisi sote na umma mzima wa Kiislamu katika dua zake za heri na zinazojibiwa. Ibariki dunia kwa ujio wake kwa sababu nyoyo zetu zimejaa yakini kutokana na hadi hiyo ya kweli. Kama unavyosema mwenyewe. "Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu."
Salamu, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya ndugu na dada zetu Waislamu.
Seyyed Mujtaba Hosseini Khamenei
Khordad 5, 1405
Dhul- Hijja 9, 1447
(May 26,2026)