Meja Jenerali Ataollah Salehi: Marekani ni adui nambari moja wa taifa la Iran
(last modified Mon, 21 Nov 2016 14:12:03 GMT )
Nov 21, 2016 14:12 UTC
  • Meja Jenerali Ataollah Salehi: Marekani ni adui nambari moja wa taifa la Iran

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani ni adui nambari moja wa taifa la Iran na ni tishio kwa mataifa yote ya Mashariki ya Kati.

Meja Jenerali Ataollah Salehi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amesema hayo leo katika hafla ya kumuaga Brigedia Jenerali Ahmad Reza Pourdastan, Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kumtambulisha kamanda mpya wa jeshi hilo Brigedia Jenerali Kiumars Heidari na kubainisha kwamba, katika miaka ya hivi karibuni, Iran mara kadhaa imezitahadharisha nchi za Mashariki ya Kati kuhusiana na siasa za Marekani, mauaji na uharibifu unaoshuhudiwa hii leo katika nchi za eneo hili.

Meja Jenerali Ataollah Salehi sambamba na kubainisha kwamba, katu Marekani haiwezi kuwa na uhusiano wa kirafiki na Iran amesema kuwa, kuweko Kiongozi mwenye busara na uwezo wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mambo ambayo yameifanya nguvu ya mabavu ya Marekani kutofanya kazi.

Brigedia Jenerali Kiumars Heidari, Kamanda mpya wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Ameongeza kuwa, watu wote wanatambua kwamba, adui Marekani anatafuta fursa ili atoe pigo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Meja Jenerali Ataollah Salehi Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuzigawa nchi za Mashariki ya Kati ikiweko Iraq, Syria, na Yemen ni miongoni mwa malengo ya siasa za Marekani ya kuanzisha vita vya niaba katika eneo la Mashariki ya Kati.

Aidha Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mpango huo wa Marekani utashindwa na kundi la kigaidi la Daesh litaangamizwa muda si mrefu.