Dakta Larijani: Israel ni mama wa ugaidi duniani
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika kumbukumbu za karne za mwisho hakuna tukio baya kama la kuasisiwa utawala haramu wa Israel kwani kuanzishwa na kuundwa utawala huo kumepelekea kufanyika jinai ambazo hazijawahi kutokea katika historia.
Dakta Ali Larijani alisema hayo jana katika hotuba aliyotoa kabla ya hotuba za Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kubainisha kwamba, suala la himaya kwa kadhia ya Palestina ni wadhifa na jukumu la Kiislamu na kuongeza kuwa, lengo la Imam Khomeini (MA) la kuiainisha na kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds lilikuwa ni kuyaamsha mataifa ya Kiislamu na kuyafanya yasighafilike na jukumu muhimu la Kiislamu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kwamba, kuundwa utawala haramu wa Israel kulikuwa mwanzo wa kuanza ukosefu wa usalama na amani katika Mashariki ya Kati na utawala huu hii leo ambao unaunga mkono magaidi waziwazi umezifanya nchi nyingi za Kiislamu kupigana.
Amesema, ardhi ya Palestina na Quds Tukufu kilikuwa kituo cha Mitume na Wahyi wa Mwenyezi Mungu na eneo ambalo linaheshimiwa na Waislamu na wafuasi wa dini zote za mbinguni.
Dakta Larijani amebnainisha kuwa, utawala wa Kizayuni wea Israel ni mama wa ugaidi na kwamba, jinai za utawala huo ghasibu hazina mfano katika historia.
Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa, himaya ya Marekani kwa utawala vamizi wa Israel ina maana kwamba, washington ni mfuasi wa mama wa magaidi.