Iran na Misri kuimarisha ushirikiano wao wa mabunge
(last modified Tue, 06 Feb 2018 07:16:55 GMT )
Feb 06, 2018 07:16 UTC
  • Iran na Misri kuimarisha ushirikiano wao wa mabunge

Hossein Amir-Abdollahian, msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesisitizia umuhimu wa kuimarishwa uhusiano wa mabunge ya nchi hii na Misri.

Abdollahian aliyasema hayo jana Jumatatu hapa mjini Tehran, alipokutana na kufanya mazungumzo na afisa mkuu anayeshughulikia maslahi ya Misri hapa nchini na kusisitiza kuwa ushirikiano wa mabunge ya nchi mbili hizi ni jambo lenye umuhimu mkubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa na mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Misri kadhalika wamezungumzia masuala yenye maslahi ya pande mbili.

Bendera za Iran na Misri

Maafisa hao wa Iran na Misri wamesema ushirikiano wa mabunge ya nchi mbili hizi unaweza kuwa kigezo katika kuipatia ufumbuzi migogoro inayolikabili eneo hili, hususan ufumbuzi wa kisiasa.

Aidha wawili hao wamesisitizia haja ya kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili katika nyuga mbali mbali.

Kadhalika maafisa hao wa ngazi za juu wa Iran na Misri wamesisitizia udharura wa kulitetea na kuliunga mkono taifa huru la Palestina.

Tags