Zarif: Kikao cha Vienna kimesisitiza kuhusu kudhaminiwa maslahi ya taifa la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46605-zarif_kikao_cha_vienna_kimesisitiza_kuhusu_kudhaminiwa_maslahi_ya_taifa_la_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema maslahi ya taifa la Iran lazima yadhaminiwe kwa mujibu wa mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji, JCPOA, na hilo ni jambo ambalo pia madola matano yaliyosalia katika JCPOA yanasisitiza.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 06, 2018 14:22 UTC
  • Zarif: Kikao cha Vienna kimesisitiza kuhusu kudhaminiwa maslahi ya taifa la Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema maslahi ya taifa la Iran lazima yadhaminiwe kwa mujibu wa mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji, JCPOA, na hilo ni jambo ambalo pia madola matano yaliyosalia katika JCPOA yanasisitiza.

Mohammad Javad Zarif ameyasema hayo leo mjini Vienna Austria baada ya kumalizika mkutano wa Tume ya Pamoja ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi zilizosalia katika JCPOA. Kikao hicho kimewaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pamoja na mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya. Hicho kilikuwa kikao cha kwanza cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoafiki JCPOA tokea Marekani ijiondoa katika mapatano hayo mnamo Mei 8.

Zarif amesema kikao hicho kilikuwa chanya na chenye uzito mkubwa na kwamba katika kipindi cha miezi miwili tokea Marekani ikiuke sheria na kijiondoa katika JCPOA, kumefanyika jitihada za kudhamini maslahi ya kiuchumi ya Iran katika fremu ya JCPOA.
Zarif ameogneza kuwa, Iran iliombwa na nchi zilizosalia JCPOA iahirishe hatua dhidi ya ukiukwaji uliotekelezwa na Marekani ili nchi hizo zipate fursa ya kujadili njia za kudhamini maslahi ya Iran.

Zarif ameongeza kuwa nchi hizo zilizosalia katika JCPOA, kupitia taarifa ya mwisho ya kikao hicho iliyosomwa na Federica Mogherini mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya, zimesisitiza kuhusua masuala kama vile kuendelea kuuzwa mafuta ghafi ya Iran, uhusiano wa kibenki, uchukuzi, ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.

Mkutano wa Tume ya Pamoja ya JCPOA, Vienna, Austria 06/07/2018

Aidha Zarif ameashiria hotuba ya Rais Rouhani wa Iran ambaye amesema kifurishi cha mapendekezo ya Ulaya kwa Iran kuhusu kubakia katika JCPOA ni cha kuvunja moyo na kusema: "Hadi sasa tatizo lililoibuka baada ya Marekani kujiondoa JCPOA bado halijatatuliwa. Kwa hivyo Iran ina haki ya kuchukua hatua kwa ajili ya kulinda maslahi yake.

Katika taarifa baada ya kumalizika mkutano wa Tume ya Pamoja ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi zilizosalia katika JCPOA, mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema pande husika zimeafiki kuendeleza mazungumzo kwa ajili ya kuokoa mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA.