Qassemi: Hakuna imani yoyote ya kufanya mazungumzo na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47294-qassemi_hakuna_imani_yoyote_ya_kufanya_mazungumzo_na_marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuhusu matamshi ya karibuni ya rais wa Marekani kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwamba: kutokana na sera za Marekani za kuendesha vita vikubwa vya kisaikolojia dhidi ya Iran hakuna dhamana wala imani yoyote juu ya serikali ya Marekani wala rais wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 07, 2018 10:08 UTC
  • Qassemi: Hakuna imani yoyote ya kufanya mazungumzo na Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuhusu matamshi ya karibuni ya rais wa Marekani kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwamba: kutokana na sera za Marekani za kuendesha vita vikubwa vya kisaikolojia dhidi ya Iran hakuna dhamana wala imani yoyote juu ya serikali ya Marekani wala rais wa nchi hiyo.

Bahram Qassemi ameashiria kuwa Iran ni nchi yenye nguvu na uwezo na wala haina kiwewe chochote cha kufanya mazungumzo na akabainisha kwamba, vipi anaweza kudai kuwa anataka mazungumzo mtu ambaye amejichukulia kivyake na kwa upande mmoja uamuzi wa kujitoa kwenye makubaliano kama JCPOA huku akiwa haungwi mkono kwa namna yoyote ile hata na washirika wake wa jadi.

Rais wa Marekani Donald Trump amedai hivi karibuni kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran "bila masharti yoyote".

Rais wa Marekani Donald Trump

Huku akiashiria kwamba msimamo huo uliotangazwa hivi karibuni na Trump wa kufanya mazungumzo na Iran umezusha mkanganyo kwa viongozi wa baadhi ya nchi hasimu za eneo pamoja na utawala wa Kizayuni, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebainisha kuwa: Trump anatumia mbinu hiyo ili kuweza kuchota fedha zaidi kutoka kwa utawala wa Kizayuni ulioighusubu Quds na baadhi ya nchi zinazofuata misimamo yake.../