Sep 08, 2018 01:22 UTC
  • Zarif: Mapatano ya kumaliza ugaidi na mateso ya wananchi wa Idlib Syria yameshafikiwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika kikao cha pande tatu za Iran, Russia na Uturuki kilichofanyika hapa Tehran jana Ijumaa, kumefikiwa mapatano ya kumaliza ugaidi na mateso ya wananchi wa mkoa wa Idlib, nchini Syria.

Baada ya kumalizika kikao cha pande hizo tatu, Mohammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Wakati ambapo rais wa Marekani Donald Trump anawadhalilisha waitifaki wake kwa michezo yake ya kitoto na kupoteza heshima na itibari ya nchi hizo, Iran inafanya mazungumzo na madola yenye nia ya kweli ya kuupatia suluhisho la kisiasa mgogoro wa Syria.

Mji wa Idlib ulivyoharibiwa vibaya na magaidi

 

Kikao cha pande tatu cha marais wa Iran, Russia na Uturuki kimefanyika hapa Tehran kwa ajili ya kufuatilia mchakato wa kisiasa wa kutatua mgogoro wa Syria katika wakati huu wa kukaribia kukombolewa kikamilifu mkoa wa Idlib, moja ya maeneo ya mwisho kabisa ya Syria ambayo bado yamo mikononi mwa magenge ya magaidi wakufurishaji.

Syria ilivamiwa kila upande mwaka 2011 na magenge ya kila namna ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao kwa lengo la kuupindua serikali halali ya nchi hiyo na kubadilisha mlingano wa nguvu katika eneo hili kwa faida ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Hata hivyo njama hizo zote zimeshindwa na hivi sasa magenge ya kigaidi yamekaribia kusafishwa kikamilifu nchini Syria. Ni vyema kusema hapa kuwa, mgogoro huo waliotwishwa wananchi wa Syria na madola dhalimu ya kigeni umepelekea mamilioni ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu kuwa wakimbizi.

Tags