Jun 27, 2024 12:29 UTC
  • Tehran, mwenyeji wa mkutano wa nafasi ya utambulisho wa asili na muqawama katika kuasisi mfumo mpya duniani

Mkutano wa kimataifa uliofanyika chini ya anwani ya "Nafasi ya Utambulisho wa Asili na Muqawama Katika Kuasisi Mfumo Mpya Duniani" umefanyika leo hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na wataalamu na wanafikra wa kimataifa.

Miaka mitatu iliyopita kitengo cha matangazo ya nje katika Shirika la Utangazaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kilizindua wazo la kufanyika "Tamasha la Asubuhi", ambalo lilikaribishwa na kuungwa mkono pakubwa dani na nje ya nchi, na kwa mtazamo huo, "Kituo cha Mafunzo cha Sobh" kiliasisiwa kwa lengo la kufikisha sauti ya mfumo mpya wa dunia kwa walimwengu. 

Shirika la habari la Iran Press limeripoti kuwa, Ahmad Nouruzi Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Matangazo ya Nje cha Sauti na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo katika mkutano huo kwamba huo ni mkutano wa kwanza wa utafiti wa Kituo cha Sobh, ambacho kinajaribu kuchukua hatua za kivitendo kuanzisha mawasiliano kati ya wawakilishi wa vyombo vya habari. 

Nourozi ameashiria dhana ya  "New World Order" na akasema: Mauaji ya kimbari yanaendelea Ukanda wa Gaza kwa miezi nane sasa na utawala wa Kizayuni unaendeleza jinai zake dhidi ya eneo hilo kwa himaya na uungaji mkono wa Marekani. Mauaji  ya kimbari yanayoendelea Ukanda wa Gaza yameathiri muundo mpya wa dunia huku mhimili wa muqawama ukipenya katika maeneo ya mipaka na sasa Palestina imekuwa kitovu cha duara la muundo mpya wa dunia.  

Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza 

Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Matangazo ya Nje cha Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB) pia amesema: Hivi sasa ambapo mkutano huu umefanyika baada ya kufa shahidi Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir Abdollahian  na wenzao wengine hatuwezi kupuuza mchango wa mashahidi hawa wawili katika kuasisi muundo mpya wa dunia; na kuna matumaini ya kuendelezwa na kufikia natija  njia hii iliyoanzishwa na mashahidi hawa. 

Tags