Oct 26, 2018 15:19 UTC

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema stratijia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuimarisha uwezo wake wa kujihami ni kwa shabaha ya kuzuia vita katika eneo hili la Mashariki ya Kati.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Mohammad Hasan Aboutorabifard ameyasema hayo katika hotuba za swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran na kubainisha kwamba, uwezo mkubwa wa kijeshi wa Iran hautairuhusu Marekani kufikia malengo yake haramu, ambayo ni kuchochea vita katika ulimwengu wa Kiislamu.

Amebainisha kuwa, utawala wa ukoo wa Aal Saud unaochukiwa kote duniani hivi sasa na ambao unakingiwa kifua na Marekani hautaweza kueneza sera zake za kuchochea vita katika eneo hili, kutokana na ushawishi na uwezo wa mataifa ya Kiislamu kama vile Iran, Iraq, Lebanon, Syria, Yemen na Palestina. 

Makombora ya balestiki ya Iran

Sayyid Mohammad Hasan Aboutorabifard vile vile ameashiria vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran vinavyotazamiwa kuanza kutekelezwa Novemba 5 mwaka huu na kusisitiza kuwa, hatua hiyo ya Washington ya kutangaza vikwazo hivyo si tu imekumbwa na pingamizi kutoka Tehran pekee bali kutoka kwa nusu ya jamii ya kimataifa.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amefafanua kuwa, vikwazo hivyo vya kidhalimu vya Marekani vitaiongezea nguvu na ushawishi Jamhuri ya Kiislamu, taifa ambalo litasambaratisha sera za vita za Washington.

 

Tags