Mar 15, 2019 07:20 UTC
  • Iran: Serikali ya Marekani ndiyo mkiukaji mkubwa kabisa wa haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Serikali ya Marekani ndiyo mkiukaji mkubwa kabisa wa haki za binadamu za wananchi wa Iran, kwani kwa kuwatwisha vikwazo vyake haramu vya nje ya mipaka na vya upande mmoja, Washington haijasita kuchukua hatua yoyote ya kukanyaga haki za raia wa Iran.

Bahram Qassemi ametoa kauli hiyo jana kujibu ripoti ya kila mwaka ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu hali ya haki za binadamu katika nchi nyingine duniani na kufafanua kwamba: Serikali ya Marekani inatoa ripoti ya kila mwaka ya haki za binadamu na kuzielekezea nchi zingine kidole cha tuhuma, ilhali yenyewe ina faili zito la ukiukaji haki za binadamu ndani na nje ya ardhi yake, na kila mara inalaumiwa na kukosolewa vikali na nchi nyingi, fikra za waliowengi, asasi za kiraia, wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu, Umoja wa Mataifa, maripota maalumu wa umoja huo na hata ndani ya Marekani kwenyewe.

Ukandamizaji na ukiukaji haki za binadamu wa askari wa Marekani katika mji wa Ferguson nchini humo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, masuala yaliyoashiriwa katika ripoti ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran yametokana na uchambuzi potofu, wa chuki na wenye utashi wa kisiasa kuhusu baadhi ya matukio ya haki za binadamu yaliyojiri nchini, ambapo kwa kuzingatia faili na rekodi yake chafu na isiyoweza kutetewa ya haki za binadamu, ni wazi kwamba Washington haina ustahiki wa kuzungumzia masuala hayo.../ 

Tags