Rais Rouhani: Iran imesambaratisha chuki dhidi ya Uislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i5395-rais_rouhani_iran_imesambaratisha_chuki_dhidi_ya_uislamu
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa kubwa la Iran limesambaratisha njama za madola makubwa na Wazayuni za kueneza chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Iran
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 19, 2016 10:58 UTC
  • Rais Rouhani: Iran imesambaratisha chuki dhidi ya Uislamu

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa kubwa la Iran limesambaratisha njama za madola makubwa na Wazayuni za kueneza chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Iran

Rais Rouhani ameyasema hayo leo Jumanne alipohutubia halaiki kubwa ya watu katika mkoa wa Semnan mashariki mwa Iran na kuongeza kuwa: "Taifa la Iran limeibuka mshindi mbele ya mashinikizo yote ya vikwazo na matatizo ya kieneo na kimataifa."

Rais Rouhani ameashiria mapatano ya nyuklia baina ya Iran na madola makubwa duniani ya kundi la 5+1 sambamba na kutekekelezwa mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kusema: "JCPOA ni fakhari ya kisiasa na kisheria kwa taifa la Iran."

Rais wa Iran ameongeza kuwa, kufuatia mapatano hayo maazimio sita ya Baraza la Usalama na 12 ya Bodi ya Magavana wa IAEA dhidi ya Iran yameondolewa.

Aidha amekosoa wale wanaodai kuwa taifa la Iran halijapata ushindi na kwamba Marekani ndie mshindi katika mapatano ya nyuklia.

Rais Rouhani amesema vikwazo vimeondolewa na uhusiano na Iran na benki za dunia unafunguliwa hatua kwa hatua. Amesema wafanya biashara wa Iran wanaweza kuuza bidhaa nje lakini amesema itachukua muda wawekezaji wa kigeni kuja Iran.