Ayatullah Khamenei ateua wajumbe wapya wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76910-ayatullah_khamenei_ateua_wajumbe_wapya_wa_baraza_kuu_la_mapinduzi_ya_kiutamaduni
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameteua wajumbe wapya wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2021 12:40 UTC
  • Ayatullah Ali Khamenei
    Ayatullah Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameteua wajumbe wapya wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei imesema kuwa, katika dikrii yake ya kuteua wajumbe wapya wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni, Ayatullah Khamenei amewashukuru wajumbe wa zamani wa baraa hilo ambao hawatakuwemo katika baraza jipya na kusema: Muundo jumla wa utamaduni unaozingatia mfumo wa Mapinduzi ndiyo njia pekee ya kujikinga na hujuma ya kitamaduni na ya vyombo vya habari vya kigeni.

Dikri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema: Kuingia katika arobaini la pili la Mapinduzi ya Kiislamu, ambako kunasadifiana na mwanzo wa karne mpya Hijria Shamsia, kunazidisha udharura wa kuwepo mtazamo mpya, wa kiutafiti na wa kisasa wa majmui ya miundomsingi ya ustaarabu.

Amesema majmui muhimu zaidi kati ya seti hizo ni utamaduni na kuongeza kuwa: Utamaduni ndio injini inayoelekeza na kuongoza hatua zote za kimsingi na miundomsingi ya jamii ya mwanadamu ambayo ndiyo inayotia kasi au kupunguza kasi ya hatua hizo. Ameongeza kuwa kwa sasa mwelekeo huo unalenga kustawisha mtazamo na uwajibikaji wa maafisa wa sekta ya utamaduni, wasomi na wanaharakati wa nyanja mbalimbali hapa nchini katika kadhia ya utamaduni na kuibua imani madhubuti kwamba, kuimarisha utamaduni katika kila moja katika sehemu zote za ustaarabu wa jamii ndiyo wenzo bora zaidi wa maendeleo na mafanikio yake.

Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, jukumu la tangu mwanzoni la Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni ni kuratibu hali ya utamaduni na maarifa nchini, kupanga sera za masuala hayo mawili, kuongoza taasisi husika kuelekea kwenye thamani na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu, kukukidhi mahitaji ya kifikra ya asasi hizo na kuwa kituo kikuu cha utamaduni hapa nchini.