Mabadilisho ya kibiashara ya Iran na nchi jirani yapindukia dola bilioni 28
Msemaji wa Idara ya Forodha ya Iran amesema kuwa, mabadilishano ya kibiashara baina ya Iran na nchi jirani zake imefikia dola bilioni 28 na milioni 300.
Sayyid Rouhollah Latifi amenukuliwa na shirika la habari la IRNA akisema hayo na kuongeza kuwa, kiwango cha mabadilishano ya biashara baina ya Iran na nchi jirani katika kipindi cha miezi saba iliyopita kimefikia tani milioni 61 na laki 4 na 66,000 na thamani yake ni dola bilioni 28 na milioni 300.
Ameongeza kuwa, katika kipindi cha miezi hiyo saba iliyopita, tani milioni 47 na laki 8 na 85,000 za bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 14 na milioni 782 na na laki 7 na 36,454 zimesafirishwa kutoka Iran kwenda katika nchi 15 jirani na zina uzito wa asilimia 64 na thamani ya asilimia 55 ya bidhaa zote zilizosafirishwa nje ya Iran katika kipindi cha miezi 7 iliyopita.
Msemaji huyo wa Idara ya Forodha ya Iran vile vile amesema, nchi za Iraq, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Afghanistan na Pakistan ndizo nchi tanu zinazopokea kiwango kikubwa zaidi cha bidhaa za Iran.
Ameongeza kuwa, katika kipindi hicho cha miezi saba iliyopita, Umoja wa Falme za Kiarabu umeongeza kiwango cha bidhaa unazoingiza kutoka Iran. Amesema, tani milioni 6 na laki 8 na 69,881 za bidhaa za Iran zenye thamani ya dola bilioni 8 na milioni 595 na laki 5 na 20,927 zimefanyiwa muamala baina ya Iran na Imarati pekee katika kipindi hicho cha miezi saba iliyopita.