Balozi wa Uswidi nchini Iran aitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83160-balozi_wa_uswidi_nchini_iran_aitwa_katika_wizara_ya_mambo_ya_nje
Kufuatia kuendelea kuzuiliwa kisiasa na kinyume cha sheria Hamid Nouri, raia wa Iran huko mjini Stockholm, Uswidi, balozi wa nchi hiyo mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na kuelezewa malalamiko ya Tehran kuhusu suala hilo.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
May 02, 2022 02:15 UTC
  • Balozi wa Uswidi nchini Iran aitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje

Kufuatia kuendelea kuzuiliwa kisiasa na kinyume cha sheria Hamid Nouri, raia wa Iran huko mjini Stockholm, Uswidi, balozi wa nchi hiyo mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na kuelezewa malalamiko ya Tehran kuhusu suala hilo.

Raia huyo wa Iran anashikiliwa na maafisa wa Uswidi kutokana na tuhuma bandia na za kisasa alizoelekezewa na mwendesha mashta wa nchi hiyo.

Kufuatia hali hiyo, balozi wa Uswidi mjini Tehran, Matthias Lentz, aliitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran jana Jumapili na kufahamishwa malalamiko makali ya Iran dhidi ya tuhuma zisizo na msingi na za uzushi zilizotolewa na mwendesha mashtaka wa Uswidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Peyman Saadat, Naibu Waziri na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Ulaya Magharibi katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kesi bandia na kuwekwa kizuizini Hamid Nouri ni jambo linalofanyika kinyume cha sheria na ambalo limetokama na uchochezi unaofanywa na kundi la kigaidi la Munafiqeen linalopinga Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Iran imelaani vikali hatua hiyo ya maafisa wa Uswidi dhidi ya Hamid Nouri pamoja na matamshi yanayotolewa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu katika uwanja huo.

Mkurugenzi Mkuu huyo ametaka kusimamishwa mara moja kwa kesi hiyo bandia na ya kisiasa na kuachiliwa huru Hamid Nouri.

Balozi wa Uswidi ameahidi kuwafikishia wakubwa zake katika wizara ya mambo ya nje malalamiko hayo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.