Nchi 47 zinanunua bidhaa za "nanoteknolojia" za Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i87594-nchi_47_zinanunua_bidhaa_za_nanoteknolojia_za_iran
Taarifa ya Makao Makuu Maalum kwa ajili ya Maendeleo ya Nanoteknolojia nchini Iran imesema Bidhaa za "nanoteknolojia" za Iran sasa zitauzwa katika nchi 47 ambazo zimetuma maombi ya kupokea bidhaa hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 30, 2022 03:17 UTC
  • Nchi 47 zinanunua bidhaa za

Taarifa ya Makao Makuu Maalum kwa ajili ya Maendeleo ya Nanoteknolojia nchini Iran imesema Bidhaa za "nanoteknolojia" za Iran sasa zitauzwa katika nchi 47 ambazo zimetuma maombi ya kupokea bidhaa hizo.

Taasisi hiyo imeongeza kuwa: Bidhaa na huduma za nanoteknolojia katika nyanja mbalimbali za ujenzi, optoelectroniki, dawa, afya na tiba, vitambaa na nyanja nyingine za teknolojia zinasafirishwa katika nchi 47 zilizoomba.

Iran ni miongoni mwa nchi tajika katika uga wa teknolojia ya nano katika ngazi ya kimataifa, na wanateknolojia Wairani wameweza kurekodi mafanikio muhimu katika uwanja huo.

Sekta hii, kwa msaada na uwezo wa wataalamu wa ndani ya nchi, imeweza kuharakisha njia yake ya maendeleo na kufanya bidhaa na huduma zake kuwa na ufanisi Iran na kimataifa.

Satalaiti ya Nano iliyoundwa Iran

Kwa mujibu wa ripoti ya Makao Makuu Maalum kwa ajili ya Maendeleo ya Nanoteknolojia katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Sayansi na Teknolojia, bidhaa na huduma za nanoteknolojia za makampuni ya Iran yanayotumia maarifa katika nyanja mbalimbali za ujenzi, optoelectroniki, dawa, afya na tiba, nguo na teknolojia nyinginezo zimesafirishwa katika nchi 47 ambazo zimeomba bidhaa hizo. Kati ya na nchi zilizoomba bidhaa hizo ni pamoja na Uturuki, Iraq, Lebanon, Afghanistan, Georgia, Syria, Russia, Pakistan, Tajikistan, India na Kazakhstan.

Kiasi kikubwa zaidi cha mauzo ya nano ya Iran ni kwa Uturuki yenye thamani ya dola milioni 13, Iraq yenye thamani ya dola milioni 12 na Lebanon yenye thamani ya dola milioni 3.4 mtawalia. Afghanistan, Georgia na Syria ndizo zinazofuata.

Sehemu kubwa zaidi ya mauzo ya nje ya bidhaa za nano za Iran inahusiana na sekta ya ujenzi, ambayo inachukua asilimia 53%.