Ujumbe wa mazungumzo wa Iran kurudi Vienna karibuni hivi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i90008-ujumbe_wa_mazungumzo_wa_iran_kurudi_vienna_karibuni_hivi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na mkuu wa timu ya Ira katika mazungumzo ya nyukia amegusia jinsi Marekani inavyoendeleza vikwazo vya kidhulma dhidi ya taifa hili la Kiislamu na kusema kuwa, vikwazo hivyo ni uvunjaji mkubwa sana wa haki za binadamu duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2022 03:28 UTC
  • Ujumbe wa mazungumzo wa Iran kurudi Vienna karibuni hivi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na mkuu wa timu ya Ira katika mazungumzo ya nyukia amegusia jinsi Marekani inavyoendeleza vikwazo vya kidhulma dhidi ya taifa hili la Kiislamu na kusema kuwa, vikwazo hivyo ni uvunjaji mkubwa sana wa haki za binadamu duniani.

Ali Bagheri amegusia pia shambulio la kigaidi la hivi karibuni lililofanywa na maadui wa taifa hili katika haram ya Shah Cheragh iliyoko Shiraz, kusini magharibi mwa Iran na ambalo liliua na kujeruhi makumi ya watu wasio na hatia na kuongeza kuwa, shambulio la kigaidi la mjini Shiraz ni ushahidi mwingine kwamba msimamo wa taifa la Iran ni wa haki katika kusimama imara kukabiliana na misimamo ya kuchupa mipaka, ukati, kutumia mabavu na ugaidi wa Daesh (ISIS) kwenye eneo hili.

Amezungumzia pia siasa za kindumilakuwili za madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani katika suala zima la kupambana na ugaidi na kusisitiza kuwa, hadi hivi sasa baadhi ya nchi hizo za Magharibi zimeshindwa hata kusema tu kuwa zimehuzunishwa na shambulio la kigidi la mjini Shiraz. Zimeshindwa hata kulaani kwa maneno tu shambulizi hilo la kikatili. Nchi hizo hazimuonei huruma hata mtoto mdogo ambaye amepoteza baba yake, mama yake na kaka yake katika shambulio hilo la kigaidi.

Maziko ya wahanga wa shambulio la kigaidi la Shah Cheragh mjini Shiraz, Iran

 

Amma kuhusu mazungumzo ya kuondolewa vikwazo Iran, Bagheri amesema, siku zilizopita, Tehran ilifanya ubunifu mwingine kwa shabaha ya kutia kasi mazungumzo hayo na inatumai kwamba ubunifu wake huo utaandaa mazingira ya kuchukuliwa hatua mpya katika mazungumzo hayo.

Vile vile amesema, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa, timu ya wataalamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itapelekwa mjini Vienna Austria karibuni hivi kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kujadiliana na maafisa wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA.