Maandamano ya Yaumu-Llah Aban13 yafanyika kila pembe ya Iran ya Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i90048-maandamano_ya_yaumu_llah_aban13_yafanyika_kila_pembe_ya_iran_ya_kiislamu
Maandamano ya Yaumu-Llah Aban 13 inayosadifiana na Novemba 4 yameanza mbele ya Pango la Ujasusi la uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran sambamba na miji mingine 900 nchini kwa kuhudhuriwa na wanafunzi, wanachuo na wananchi wa matabaka mbalimbali.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Nov 04, 2022 03:54 UTC
  • Maandamano ya Yaumu-Llah Aban13 yafanyika kila pembe ya Iran ya Kiislamu

Maandamano ya Yaumu-Llah Aban 13 inayosadifiana na Novemba 4 yameanza mbele ya Pango la Ujasusi la uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran sambamba na miji mingine 900 nchini kwa kuhudhuriwa na wanafunzi, wanachuo na wananchi wa matabaka mbalimbali.

Miaka 43 iliyopita katika siku hii (Aban 13, 1358, sawa na Novemba 4, 1979), wanachuo wa vyuo vikuu vya Iran waliliteka Pango la Ujasusi la Marekani (Ubalozi) mjini Tehran kulalamikia njama kadhaa wa kadhaa zilizokuwa zikifanywa na Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Tarehe 13 Aban, sawa na Novemba 4 ni kumbukumbu ya matukio matatu muhimu katika vipindi vitatu nyeti na hasasi vya historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Matukio hayo matatu muhimu ya kumbukumbu ni siku aliyobaidishwa na kupelekwa uhamishoni nchini Uturuki Imam Khomeini (MA) tarehe 4 Novemba 1964, siku waliyouliwa wanafunzi na askari wa utawala wa Pahlavi Novemba 4, 1978 na siku ilipofanyika harakati ya kimapinduzi ya kuliteka Pango la Ujasusi la uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran.

Maandamano ya Aban 13, Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari

Harakati hiyo ya Novemba 4, 1979 ilitekelezwa na wanachuo wafuasi wa njia ya Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kila moja kati ya matukio hayo matatu ilikuwa hatua muhimu sana katika mchakato wa harakati za taifa la Iran za kupambana na Uistikbari.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, washiriki wa maandamano ya leo ya kupinga Uistikbari wanapiga nara za "Mauti kwa Marekani" kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kiuadui na kiistikbari za Mfumo wa Ubeberu unaoongozwa na Marekani mtenda jinai.

Mjini Tehran, maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari yanaishia mbele ya Pango la Ujasusi la zamani la uliokuwa ubalozi wa Marekani kwenye Mtaa wa Taleghani; na Seyyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ndiye atakayehutubia hafla hiyo.../