Apr 01, 2023 04:53 UTC
  • Mkono wa pole kwa mnasaba wa kuaga dunia Bibi Khadija, mke mtukufu wa Mtume (saw)

Tarehe 10 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani Hijiria Qamaria, ambayo inasadifiana na tarehe Mosi Aprili 2023 ni siku ya kukumbuka kuaga dunia Bibi Khadija (sa) , mke mtukufu wa Mtume Muhammad (saw).

Bi Khadija (sa) ambaye alikuwa mmoja wa wanawake mashuhuri na matajiri zaidi wa ukoo wa Quraish mjini Makka aliolewa na Mtume Mtukufu, miaka 15 kabla ya kubaathiwa kwake (saw).

Bibi huyo mtukufu alikuwa mwanamke wa kwanza kusilimu na kumwamini Mtume (saw) ambapo alitumia uwezo na utajiri wake wote katika keneza na kufanikisha malengo ya dini tukufu ya Uislamu.

Hata kabla ya kudhihiri Uislamu, Bibi Khadija alikuwa na sifa nzuri sana na za kupigiwa mfano ambapo jambo hilo lilimpeleka kupewa lakabu ya Twahira.

Bibi Khadija

Uwepo wa Bibi Khadija (sa) ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa Mtume kadiri kwamba alitija kuaga kwake kuwa ni msiba mkubwa na kuuita mwaka huo ambapo pia aliga dunia muungaji mkono na mtetezi wake mwingine mkubwa yaani Abu Talib (as) ambaye alikuwa ami yake kuwa ni Mwaka wa Huzuni.

Bibi Khadija alijaaliwa kuwa na watoto sita ambapo kati ya hao Bibi Fatwima (as) ana hadhi na fadhila maalumu katika Uislamu. Binti huyo mtukufu (as) aliolewa na Imam Ali, ambaye ni Imam wa kwanza wa Maisha na hivyo kuchukua uongozi wa Waislamu baada ya kuaga dunia Mtume Mtukufu (saw), kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mwenyewe.

Kwa mnasaba huu mchungu, Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa mkono wa pole kwa Waislamu wote duniani na hasa wafuasi na wapenda Watu wa Nyumba ya Mtume Mtukufu (saw).

Tags