Apr 02, 2023 10:52 UTC
  • IRGC yasisitiza: Jinai ulizofanya utawala wa Kizayuni katu hazitaachwa bila kujibiwa

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesisitiza kuwa: bila ya shaka yoyote jinai za utawala bandia na mtenda jinai wa Kizayuni hazitaachwa bila kujibiwa; na utawala huo haramu utalipa gharama za jinai zake.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetoa taarifa leo ya mkono wa pole kwa kufa shahidi Kapteni Miqdad Mehghani Jaafar Abadi, afisa muumini, mwenye ikhlasi na moyo wa kujitolea na vilevile na Meja Milad Heydari, mmoja wa washauri wa kijeshi wa IRGC nchini Syria ambaye aliuawa shahidi katika shambulio la kijinai la utawala wa Kizayuni alfajiri ya kuamkia Ijumaa lililolenga kiunga cha mji mkuu wa nchi hiyo Damascus, na kusisitiza kuwa: Utawala bandia na mtenda jinai wa Kizayuni utalipa gharama za jinai za kuishambulia kijeshi Syria.
Shahidi Miqdad Mehghani Jaafar Abadi

Shahidi Miqdad Mehghani Jaafar Abadi, mshauri wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Syria ambaye ni mpiganaji mwenzake Shahidi Milad Heydari, amekufa shahidi kutokana na majeraha aliyopata katika shambulio la Wazayuni lililolenga kiunga cha mji wa Damascus alfajiri ya kuamkia Ijumaa iliyopita.

Alfajiri ya kuamkia Ijumaa, ndege za kivita za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel zilishambulia kwa makombora maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Syria, Damascus.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Syria, eneo la Al Dimas limeshambuliwa na ndege hizo za kivita za utawala vamizi wa Kizayuni.../

 

Tags