Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran:Vyombo vya intelijinsia havitawaacha magaidi
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa vyombo vya intelijinsia havitaacha kuwasaka magaidi.
Juzi Jumamosi tarehe 8 Julai timu moja ya magaidi wanne iliyokuwa imeazimia kuvamia kituo cha polisi cha 16 katika mkoa wa Zahidan hapa nchini ilikabiliwa na polisi kituoni hapo na kushindwa kufikia lengo lake ovu la kigaidi baada ya magaidi wote kuangamizwa.
Maafisa wawili wa polisi katika kituo hicho cha polisi cha Zahidan kwa majina ya Alireza Keikha na Mobin Rashidi waliuliwa shahidi katika mapigano na magaidi hao.

Ahmad Vahidi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran jana alitoa onyo kuhusu shambulio hilo la kigaidi katika kituo cha polisi huko Zahedan makao makuu ya mkoa wa Sistan na Baluchistan kusini mashariki mwa Iran na kusema vyombo vya intelijinsia na polisi havitaacha kuyasaka makundi ya kigaidi yanayotekeleza hujuma kama hiyo ya kigaidi.
Vahidi ameongeza kusema:Tukio la Zahidan lilikuwa la kigaidi na kiuhalisia ni kwamba watu hao waliingia kama watu wa kawaida na kisha wakatekeleza hujuma ya kigaidi. "Tunataraji kuwa serikali majirani zetu watalinda mipaka na kuidhibiti, na kuwashughulikia watu wanaotoka nje ya mipaka," Amesema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran.