-
Eslami: Shughuli za nyuklia za Iran ni kwa mujibu wa kanuni za wakala wa kimataifa wa nyuklia
Dec 14, 2024 08:55Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema hadi leo, shirika hilo daima limekuwa likitekeleza shughuli za nyuklia kwa mujibu wa mkataba wa NPT wa kuzuia usambazwaji silaha za nyuklia. Aidha amesema: Shughuli ya nyuklia ya Iran zinaendelea kwa mujibu wa kanuni za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA).
-
Araghchi: "Muqawama" ndilo suluhisho pekee kwa vijana wa eneo la kukabiliana na uvamizi wa utawala wa Kizayuni
Dec 14, 2024 04:22Seyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza katika andiko lililochapishwa katika gazeti la Al-Akhbar la Syria kwamba, “Muqawama” ndio suluhisho pekee kwa vijana wa eneo hili la kukabiliana na uvamizi wa utawala wa Kizayuni.
-
Kikao cha 10 cha Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Qatar
Dec 13, 2024 23:17Kufanyika Kikao cha 10 cha Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Qatar huko Doha, kunaonyesha umuhimu unaotolewa na nchi mbili hizi kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara.
-
Waziri wa Afya: Iran ni kinara wa kikanda katika dawa za nyuklia
Dec 13, 2024 23:15Waziri wa Afya, Tiba na Elimu ya Tiba wa Iran, Mohammad Reza Zafarqandi ametangaza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ndio kinara wa kanda ya Asia Magharibi katika masuala ya nyuklia na kubainisha kuwa, kuna vituo 220 vya dawa za nyuklia katika maeneo mbalimbali ya nchi vinavyonufaika na uwezo huo na malighafi zinazozalishwa na Shirika la Atomiki la Iran.
-
Msomi wa Iran atoa wito wa kuanzishwa Umoja wa Mataifa ya Kiislamu
Dec 13, 2024 22:57Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuunda umoja na kujitahidi kuungana ili kufikia ustaarabu mpya wa Kiislamu.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Wavamizi watatimuliwa Syria
Dec 13, 2024 06:51Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria matukio ya Syria na kusema muqawama utaimarika na kuwatimua waliovamia ardhi ya Syria na kuikalia kwa mabavu.
-
Maonyesho ya bidhaa za Maabara yafunguliwa Tehran
Dec 13, 2024 06:33Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Vifaa vya Maabara Vilivyotengenezwa nchini Iran yaliyopewa jina la 'IRAN LAB EXPO' yamefunguliwa leo Tehran.
-
Mjumbe wa Iran UN: Mgogoro wa Afghanistan ni shinikizo kwa rasilimali za Iran
Dec 13, 2024 06:31Mjumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameikosoa jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuiunga mkono Iran licha ya matatizo yanayotokana na mzozo wa nchi jirani ya Afghanistan.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Imarati wazungumza kwa simu kuhusu matukio ya eneo hili
Dec 13, 2024 03:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Falme za Kiarabu na pande mbili zimebadilishana mawazo kuhusu matukio ya eneo hili hususan Syria.
-
Iran yaipongeza IAEA kwa kukiri kuwa Israel ina silaha za nyuklia, yataka ilazimishwe kuharibu silaha hizo
Dec 13, 2024 00:11Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kimataifa na Kisheria amejibu hatua ya kukiri Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kuhusu hatari za silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni, na kuutaka wakala huo ushughulikie silaha za nyuklia za Israel na sio kuusakama mradi wa matumizi ya amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.