-
Kikao cha pili cha kamati ya pande tatu za Iran, Saudi Arabia na China chafanyika Riyadh
Nov 20, 2024 08:26Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia na China zimefanya kikao cha pili cha pande tatu huko Riyadh, Saudi Arabia kwa shabaha ya kufuatilia makubaliano yaliyofikiwa huko Beijing na kuimarisha kiwango cha ushirikiano.
-
Iran: Ni muhimu kuwepo mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya kuwahami wanawake na watoto wa Gaza na Lebanon
Nov 20, 2024 08:13Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya wanawake na familia amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya kuwahami na kuwasaidia wanawake na watoto wa Gaza na Lebanon.
-
Iran yaonya kuhusu azimio lolote dhidi ya Tehran katika kikao cha Bodi ya Magavana wa IAEA
Nov 20, 2024 04:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kuwa hatua yoyote dhidi ya Tehran katika kikao kijacho cha Bodi ya Magavana wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) itazidisha ugumu wa kurekebisha hali ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia yenye malengo ya amani ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Araqchi: Wanaotoa silaha kwa Israel wanaishutumu Iran kutuma makombora huko Russia
Nov 20, 2024 04:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Umoja wa Ulaya na Uingereza zinatumia mienendo inayokinzana dhidi ya Iran ambayo inafichua sera za undumakuwili na kukwepa wajibu wao wa kulinda haki za binadamu.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Gaza imekuwa kaburi la watoto
Nov 20, 2024 04:38Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, Ukanda wa Gaza umegeuka kuwa kaburi la watoto kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel.
-
Araqchi: Ipo nia ya dhati ya kupanua ushirikiano na Syria katika nyanja zote
Nov 19, 2024 23:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nia ya dhati ya kupanua ushirikiano kati yake na Syria katika nyanja jzote.
-
Kolivand: Iran kutuma tani 10 za misaada kwa watu wa Lebanon
Nov 19, 2024 23:08Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRCS) ameeleza kuwa shirika hilo hivi karibuni litatuma tani 10 za misaada mbalimbali iliyotolewa na wananchi wa Iran kwa ajili ya wenzao wa Lebanon.
-
Kuendelea vitendo vya uhasama vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Iran
Nov 19, 2024 10:07Katika kuendeleza hatua zake za kiuadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumatatu ya jana tarehe 18 Novemba Umoja wa Ulaya ulitoa taarifa na kuliwekea vikwazo Shirika la Meli la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo kwa kisingizio na madai yasiyo na msingi ya eti Iran kuingilia mzozo wa Ukraine.
-
Kiongozi Muadhamu: Tutaendelea kuwa pamoja na wananchi wa Lebanon na Muqawama
Nov 19, 2024 07:43Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa maneno kwa ajili ya wananchi na viongozi wa Lebanon walioko kwenye vita hivi sasa na kuwaambia kuwa, sisi hatuna tofauti na nyinyi, tuko pamoja nanyi na tutaendelea kuwa pamoja nanyi.
-
Araghchi: Iran itatoa majibu kwa Israel katika wakati itakaoona unafaa
Nov 19, 2024 07:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia jinai ya Israel ya kushambulia ardhi ya Iran na kusema kuwa Jamhuri ya Kiislamu itatoa majibu kwa utawala wa Kizayuni katika muda inaoona unafaa na kwamba Tehran bado inahifadhi haki yake ya kutoa majibu makali kwa Israel.