-
Kiongozi Muadhamu: Kufanikiwa Rais mpya wa Iran, ni mafanikio kwetu sote
Jul 21, 2024 07:33Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameiasa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) idumishe maingiliano yenye kujenga na uongozi wa Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu, Masoud Pezeshkian na kusema kuwa, mafanikio ya Rais mpya wa Iran ya Kiislamu ni mafanikio ya taifa hili zima.
-
Iran yapongeza hukumu ya ICJ, yataka kura ya maoni kuamua mustakbali wa Palestina
Jul 20, 2024 23:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, njia bora zaidi ya kulipatia ufumbuzi suala la Palestina na kukomeshwa jinai za utawala haramu wa Israel, ni kufanyika kura ya maoni itakayowashirikisha Wapalestina wa ardhi zote za taifa hilo ili waamue mustakbali wao.
-
Marekani chimbuko kuu la matatizo Asia Magharibi
Jul 20, 2024 07:03Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekosoa vikali maamuzi na hatua za mabavu na za upande mmoja zinazochukuliwa na Marekani katika masuala mbali mbali ya Asia Magharibi na kubainisha kwamba, hatua hizo ndio chimbuko kuu la matatizo yanayolikumba eneo hili.
-
Utayari wa Iran wa kushirikiana katika kuimarisha amani na usalama katika eneo
Jul 20, 2024 04:31Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Iran iko tayari kushirikiana na nchi nyingine katika fremu ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na changamoto za dharura na kuimarisha amani na usalama katika eneo.
-
Iran: Pingamizi la kuundwa taifa la Palestina limeanika dhati ya ubaguzi ya Israel
Jul 19, 2024 22:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hatua ya Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel ya kupinga kuasisiwa taifa huru la Palestina kwa mara nyingine tena imeidhihirishia dunia dhati ya ubaguzi wa rangi ya utawala huo haramu.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Shambulio la ndege zisizo na rubani huko Tel Aviv ni onyo kwa Wazayuni
Jul 19, 2024 09:36Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Shambulio la Yemen dhidi ya Tel Aviv ni onyo linaloitaka Israel ihitimishe mashambulizi ya kinyama ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.
-
Iran: US ni kizingiti katika kupatiwa ufumbuzi masuala ya ulimwengu
Jul 19, 2024 07:39Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa vikali maamuzi na hatua za mabavu na za upande mmoja zinazochukuliwa na Marekani katika masuala mbali mbali ya dunia akisisitiza kuwa, mwenendo huo unafanya hali ya mambo uliwenguni kuwa mbaya zaidi.
-
Iran yakosoa sera za kindumakuwili za nchi za Magharibi kuhusiana na jinai za Israel
Jul 19, 2024 00:22Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Iran amekosoa madai yaliyotolewa dhidi ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na misimamo ya kindumakuwili kuhusiana na maripota maalumu wa jumuiya hiyo ya kimataifa.
-
Wabunge kukutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu siku ya Jumapili
Jul 18, 2024 07:31Msemaji wa Bodi ya Uongozi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, wabunge wa bunge jipya watakutana na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu siku ya Jumapili.
-
Kanusho la Iran kwa madai ya uwongo ya Marekani ya kuhusika katika jaribio la kumuua Trump
Jul 18, 2024 07:10Baada ya tukio la kupigwa risasi Donald Trump, rais wa zamani na mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024, baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani kwa mara nyingine vikiendeleza propaganda za chuki dhidi ya Iran (Iranphobia) vilidai kuweko mkono wa Iran katika tukio hilo.