-
Iran yamuita balozi wa Italia kulalamikia hatua ya Canada dhidi ya IRGC
Jun 21, 2024 04:19Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemuita balozi wa Italia mjini Tehran ambaye anawakilisha pia maslahi ya Canada hapa nchini, kulalamikia hatua ya serikali ya Ottawa ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi".
-
Iran: Muqawama lazima uifanye Israel ilipe gharama kubwa kwa uvamizi
Jun 20, 2024 22:47Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema makundi ya muqawama yanapasa kutumia nguvu na uwezo wao wote kuufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ulipe gharama kubwa kutokana na uvamizi na mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Kani: Hatua ya Canada dhidi ya IRGC ni zawadi kwa Israel, magaidi
Jun 20, 2024 22:46Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema hatua ya Canada ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC ) kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi" ni zawadi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, magaidi na maadui wengine wa amani na uthabiti katika eneo la Asia Magharibi.
-
Bagheri Kani: Mataifa ya eneo yachukue hatua za kukomesha mauaji ya kimbari Gaza
Jun 20, 2024 09:18Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, hali ya eneo na maslahi ya mataifa ya eneo hili yanahitaji kutumia uwezo wao wote kusimamisha mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza na kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Iran yalaani hatua ya Canada ya kuliweka jeshi la SEPAH katika orodha ya magaidi
Jun 20, 2024 08:59Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani vikali hatua ya uadui ya serikali ya Canada dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).
-
Iran yajibu shutuma zisizo na msingi za Marekani kuhusu Yemen
Jun 20, 2024 03:39Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amezitaja tuhuma za Marekani dhidi ya Iran kuhusu Yemen kuwa hazina msingi wowote na kusema kwamba, Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa ikitilia mkazo utatuzi wa amani wa mgogoro wa Yemen kupitia njia za kidiplomasia.
-
Maafisa usalama wa Iran na Russia wakutana Tehran katika kikao cha pamoja
Jun 19, 2024 23:40Maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wametilia mkazo wajibu wa kushirikiana zaidi katika kupambana na ugaidi na uhalifu wa kitaasisi na kiserikali pamoja na kupambana na mihadarati.
-
Waziri Owji: US haina ubavu wa kuzuia uuzaji wa mafuta ya Iran nje ya nchi
Jun 19, 2024 08:02Waziri wa Mafuta wa Iran amesema kuwa, hakuna serikali yoyote ya Marekani yenye uwezo na ujasiri wa kuzuia uuzaji wa mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu nje ya nchi.
-
Jibu la Iran kwa taarifa ya nchi tatu za Ulaya; ni tupu, haina itibari na ni kinyume na ukweli
Jun 19, 2024 04:16Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani taarifa ya pamoja ya nchi tatu za Ulaya za Ujerumani, Uingereza na Ufaransa kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikisema kuwa ni tupu, haina itibari na ina madai yaliyo kinyume na ukweli.
-
Ahmad Vahidi: Uchaguzii ujao wa Rais wa Iran utafanyika kwa amani na usalama kamili
Jun 18, 2024 23:52Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uchaguzi ujao wa Rais hapa nchini utafanyika katika mazingira salama na ya amani kamili.