-
IRGC yapiga makao ya kamandi ya Marekani na eneo la kuegeshea droni huko Kuwait
Sep 02, 2026 12:57Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limesema kuwa vikosi vyake vimeshambulia makao makuu ya kamandi na makazi ya wanajeshi wa Marekani katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Ali Al-Salem nchini Kuwait, na kuteketeza ghala la ndege zisizo na rubani (droni) na eneo la maandalizi ya kurushia ndege hizo. Shambulizi hilo limeharibu idadi kadhaa ya ndege zisizo na rubani za jeshi la kigaidi la Marekani.
-
Qalibaf: Marekani ‘inaua kama Shetani’: Alaani shambulio dhidi ya sherehe ya harusi kusini mwa Iran
Sep 02, 2026 12:55Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf amelaani shambulio la Marekani dhidi ya sherehe ya harusi kusini mwa Iran, akisema kuwa kulenga raia katika shule, ukumbi wa michezo na sherehe ya harusi kunaonyesha namana Washington inavyotenda na kuua "kama Shetani."
-
Mbunge wa Iran ahoji namna Marekani inavyoshindwa kutofautisha shabaha za kijeshi na maeneo ya raia
Sep 02, 2026 12:53Hasan Ghashghavi, msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amehoji namna Marekani inavyoshindwa kutofautisha kati ya shabaha za kijeshi na maeneo ya raia kufuatia shambulio la majeshi ya nchi hiyo dhidi ya sherehe ya harusi huko Sirik, katika Mkoa wa Hormuzgan nchini Iran.
-
Kwa nini Marekani inaogopa kuweka vikwazo dhidi ya nchi zinazoshirikiana na Iran?
Sep 02, 2026 07:03Huku Marekani ikijaribu kuonyesha kuwa inatekeleza vita vikubwa zaidi vya kiuchumi dhidi ya Iran na kuanzisha mbwembwe zisizo na mfano wake katika uwanja huo, jambo linalojitokeza zaidi katika uhalisia wa mambo si taathira kubwa za vikwazo hivyo vinavyopigiwa debe, bali ni migongano na kuchanganyikiwa watawala wa Marekani kuhusu suala hilo.
-
IRGC yaangamiza askari wengi Wamarekani walioko Jordan baada ya US kuua raia wa Iran kwenye sherehe ya harusi
Sep 02, 2026 02:56Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimetekeleza mfululizo wa operesheni kali za kulipiza kisasi ambazo zimehusisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani zilizolenga kambi na maslahi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi kufuatia vitendo vya hivi karibuni vya utawala huo wa kigaidi vya kuanzisha uchokozi usio na sababu, ambao umepelekea kuuawa shahidi raia kadhaa wasio na hatia wa Jamhuri ya Kiislamu akiwemo mtoto mdogo.
-
Pezeshkian: Iran na Russia zinaweza kusimama kidete dhidi ya sera ya upande mmoja ya Marekani
Sep 02, 2026 02:54Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt Masoud Pezeshkian, amesema kuwa Marekani haina uhalali wowote wa kisheria wala wa kimataifa wa kuiwekea Iran vikwazo vya kidhalimu, akisisitiza kuwa Tehran na Moscow zinaweza kushirikiana bega kwa bega ili kukabiliana na sera ya upande mmoja (unilateralism) ya Marekani inayovuruga utulivu wa dunia.
-
Baqaei: Ulaya inatekeleza kivitendo maagizo ya Washington
Sep 01, 2026 14:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa sera za nchi za Ulaya za kufuata kibubusa maagizo ya Marekani akisema: "Ulaya haiwezi tena kuzungumzia 'kujitawala na kujichukulia maamuzi kimkakati' ilhali imejishusha yenyewe hadi kuwa mtekelezaji wa maagizo ya Washington.
-
Kiongozi Muadhamu awasamehe na kuwapunguzia vifungo wafungwa zaidi ya 2,500 kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume SAW
Sep 01, 2026 03:30Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ameidhinisha kusamehewa kikamilifu au sehemu ya adhabu wafungwa zaidi ya 2,500 kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume SAW.
-
Jenerali Shekarchi: Zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Israel waliuawa katika vita na Iran
Sep 01, 2026 03:28Msemaji mkuu wa vikosi vya majeshi ya Iran amesema: "Zaidi ya wanajeshi elfu moja wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuawa katika vita na Iran na maelfu yaw engine wamejeruhiwa."
-
Rais Pezeshkian: Kuna makundi nchini Marekani yanayoona maslahi yao yapo katika kuendelea vita
Aug 31, 2026 12:19Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuna makundi nchini Marekani yanayoona maslahi yao yapo katika kuendelea vita na hivyo yanataka vita viendelee.