Baqaei: Ulaya inatekeleza kivitendo maagizo ya Washington
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141126-baqaei_ulaya_inatekeleza_kivitendo_maagizo_ya_washington
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa sera za nchi za Ulaya za kufuata kibubusa maagizo ya Marekani akisema: "Ulaya haiwezi tena kuzungumzia 'kujitawala na kujichukulia maamuzi kimkakati' ilhali imejishusha yenyewe hadi kuwa mtekelezaji wa maagizo ya Washington.
(last modified 2026-09-01T14:52:42+00:00 )
Sep 01, 2026 14:51 UTC
  • Esmail Baqaei, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
    Esmail Baqaei, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa sera za nchi za Ulaya za kufuata kibubusa maagizo ya Marekani akisema: "Ulaya haiwezi tena kuzungumzia 'kujitawala na kujichukulia maamuzi kimkakati' ilhali imejishusha yenyewe hadi kuwa mtekelezaji wa maagizo ya Washington.

"Esmail Baqaei, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, aliandika Jumatatu usiku akijibu kauli ya Umoja wa Ulaya inayounga mkono vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran kwamba: "Mwandishi wa Kifaransa, de la Boissy, katika makala yenye kichwa cha maneno: "Discourse on Voluntary Servitude," anaeleza ukweli wa msingi kuhusu wale waliotayarisha mazingira ya kutokea udhalimu na ubeberu akisema: Udhibiti wa nchi moja juu ya nyingine si tu matokeo ya mabavu, lakini mara nyingi hutokea kutokana na utii na kujidunisha kwa wale wenye uwezo wa kutenda kwa kujitegemea."Baqaei amesisitiza kwa kusema: Ulaya haiwezi tena kuzungumzia "kujitawala kimkakati" ilhali imejidunisha yenyewe hadi kuwa mtekelezaji wa maagizo ya Washington.Amefafanua kwamba: Kujitawala kimkakati hakupatikani kwa kutoa kauli kubwa, bali kwa kuonyesha irada na uwezo wa kufanya maamuzi huru na yenye uwajibikaji, hata kama maamuzi haya hayaoani na misimamo ya dola kubwa zaidi.
Baqaei ameendelea kusema: "Ulaya inalazimika ichague ama kuwa mwigizaji huru, au kuzoea sana mwangwi wa siasa za upande mwingine kiasi kwamba inashindwa kumaizi baina ya mwangwi huo na kuwa huru."