-
Amr Moussa atoa indhari kali kwa Saudia na Misri kuhusiana na utawala wa kizayuni wa Israel
Jan 17, 2026 23:41Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ametoa indhari kali kwa Saudi Arabia na Misri kuhusiana na hatua zinazochukuliwa na utawala wa kizayuni wa Israel na akasema: kinachojiri hivi sasa si suala dogo na la pembeni bali ni "tishio la kimkakati" kwa usalama wa nchi za Kiarabu na eneo kwa ujumla.
-
Doumbouya, kiongozi wa kijeshi aliyegombea urais na kushinda aapishwa kuwa rais wa Guinea
Jan 17, 2026 23:40Mamady Doumbouya, jenerali aliyeongoza jeshi la Guinea kuchukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 2021, ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Marekani yatangaza wajumbe wa iitwayo 'Bodi ya Amani' ya Ghaza, yumo pia Tony Blair
Jan 17, 2026 23:09Ikulu ya White House imetangaza majina ya wajumbe wa linaloitwa baraza la amani litakaloongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump na kusimamia utawala wa eneo la Palestina la Ukanda wa Ghaza. Orodha hiyo inajumuisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mark Rubio, mjumbe maalumu wa Trump Steve Witkoff, mkwe wa Trump Jared Kushner, na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.
-
NGOs za Uingereza zaitaka serikali kusitisha mauzo yote ya silaha kwa utawala wa Israel
Jan 17, 2026 23:07Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Uingereza (NGOs) umeitaka serikali ya nchi hiyo kusitisha uuzaji wa silaha kwa utawala wa Israel, na kuonya kuwa silaha zinazotengenezwa Uingereza ziko hatarini kutumika katika mauaji ya kimbari na kuzidi kumomonyoa sheria za kimataifa.
-
Onyo la Iran kwa Marekani; Usirudie tena vita vilivyofeli vya siku 12
Jan 17, 2026 23:07Tehran imemuonya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kukariri uzoefu uliofeli wakati wa vita vya siku 12 vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
-
Tume ya Uchaguzi Uganda: Yoweri Museveni ameshinda muhula wa saba wa urais
Jan 17, 2026 11:16Tume ya uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Yoweri Kaguta Museveni kama mshindi wa Uchaguzi wa Rais uliofanyika Alhamisi wiki hii, akiwa na jumla ya kura 7,946,772 ambayo ni asilimia 71.65% ya kura zote zilozopigwa.
-
Imam Khamenei: Taifa la Iran limevunja mgongo wa fitina kwa umoja/ Lengo la Marekani ni kuimeza Iran
Jan 17, 2026 10:15Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema Iran inamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump, kama mhusika mkuu wa mauaji na uharibifu katika ghasia za hivi karibuni hapa nchini.
-
Uwezekano wa Marekani kuishambulia Mexico na nchi nyingine za Amerika Kusini
Jan 17, 2026 06:23Kufuatia kuongezeka vitisho vya Rais Donald Trump dhidi ya Mexico, maafisa wa Wizara ya Vita ya Marekani wametangaza kuwa uwezekano wa kufanyika operesheni za kijeshi nchini Mexico umeongezeka.
-
Marekani yaitengea Israel dola bilioni 3.3 nyingine za kufanyia jinai duniani
Jan 17, 2026 05:26Bunge la Marekani limepasisha muswada wa dola bilioni 3.3 kwa ajili ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao hivi sasa dunia nzima inalaani jinai zake kubwa katika maeneo tofauti hasa huko Palestina na hususan katika Ukanda wa Ghaza.
-
Chad yaelemewa na wakimbizi wa Sudan, CAR, Cameroon, Nigeria na kwengineko
Jan 17, 2026 04:40Mzigo mkubwa wa wakimbizi wanaomiminika kila leo nchini Chad umeielemea serikali ya nchi hiyo ambayo muda wote inaiomba jamii ya kimataifa na hasa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR liisaidie kubeba mzigo huo.