-
Kuondoka vikosi vya kigeni, suluhisho pekee la mgogoro wa Yemen
Jan 06, 2026 08:39Kiongozi mmoja mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, kuendelea kuwepo wanajeshi vamizi ndani ya ardhi ya Yemen ni tatizo kuu la mgogoro wa nchi hiyo akisisitiza kwamba upatanishi wowote kutoka nchi jirani hausaidii, kwani wao wenyewe hao wapatanishi ndio wahusika wakuu wa mgogoro wa Yemen.
-
Hatari za kisiasa na kiusalama za hatua ya utawala wa Israel ya kutambua rasmi Somaliland
Jan 06, 2026 07:04Kufuatia hatua ya utawala wa Israel ya kulitambua rasmi eneo la Somaliland huko Somalia kama nchi huru, kumetolewa maonyo kuhusu matokeo hatari ya kisiasa na kiusalama ya kitendo hicho.
-
Ubalozi wa Palestina wafunguliwa rasmi jijini London
Jan 06, 2026 03:38Ubalozi wa Palestina umefunguliwa rasmi jijini London, takriban miezi minne baada ya Uingereza kutangaza kuitambua Nchi ya Palestina.
-
Iran, Cuba, Brazil zataka kuheshimwa sheria za kimataifa
Jan 06, 2026 03:21Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Cuba na Brazil wamesisitiza udharura wa kuwepo ushirikiano wa karibu na uratibu miongoni mwa nchi zinazostawi katika majukwaa ya kimataifa, ili kukabiliana na mfumo wa ubeberu; na kuunga mkono sheria za kimataifa na kanuni za Hati ya Umoja wa Mataifa.
-
Touadera ashinda muhula wa 3 wa urais Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jan 06, 2026 02:59Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera ameshinda muhula wa tatu urais, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi wa karibuni, yaliyotangazwa Jumatatu na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi.
-
Baraza la Usalama lalaani hatua ya US kumteka nyara Maduro
Jan 06, 2026 02:47Wawakilishi wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiwemo waitifaki wa Marekani, wamelaani kitendo cha Washington cha kumteka nyara Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.
-
Maduro aiambia mahakama US: Ningali Rais halali wa Venezuela
Jan 06, 2026 02:40Rais wa Venezuela aliyetekwa nyara na Marekani, Nicolas Maduro ameiambia mahakama jijini New York kwamba "hana hatia", "ni mtu mstaarabu", na kwamba alikuwa "ametekwa nyara", katika matamshi yake ya kwanza hadharani tangu kujiri shambulio la kuogofya la Marekani dhidi ya nchi yake Jumamosi.
-
Iran yakanusha uvumi wa vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu mazungumzo na Marekani
Jan 06, 2026 00:06Naibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha uvunii unaoneshwa na vyombo vya habari vya Magharibi kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alifanya mkutano maalumu na waandishi wa habari siku ya Alkhamisi na kuongeza kuwa, inavyoonekana ni kwamba baadhi ya duru za Magharibi zinapenda sana kupata kisingizio cha kusema uongo na kuchochea chuki katika kila jambo.
-
Amnesty International: Serikali ya Uganda inatumia mbinu za mateso kuwatishia wapinzani
Jan 06, 2026 00:05Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limetangaza kuwa, vikosi vya usalama nchini Uganda vinatumia njia za mateso na ukamataji usio wa kisheria kuwatisha wapinzani kuelekea uchaguzi mkuu katikati ya mwezi huu wa Januari.
-
Mijibizo ya kimataifa kwa mgogoro wa Venezuela; msisitizo juu ya diplomasia, kuachiliwa Maduro, na kuhuishwa demokrasia
Jan 05, 2026 23:51Kufuatia shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya Venezuela na kukamatwa kwa rais wa nchi hiyo, viongozi mbalimbali wa dunia na serikali walionyesha wasiwasi kuhusu matokeo ya hatua hii na kutoa wito wa suluhu ya kidiplomasia ya mgogoro huo, kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa, na kurejea kwenye michakato ya kidemokrasia.