-
Madaktari Sudan watahadharisha kuhusu maafa tarajiwa ya kibinadamu huko Kordofan Kusini
Jan 04, 2026 03:35Kundi la madakatri wa Sudan limetahadharisha kuhusu maafa tarajiwa ya kiafya na kibinadamu katika mji wa Dalang unaopatikana katika jimbo la Kordofan Kusini. Kundi hilo limesema kuwa mji wa Dalang unaendelea kuzingirwa huku ukikabiliwa na mashambulizi makali ya wanagambo wa RFS.
-
Trump: Marekani ‘itajihusisha kwa nguvu’ katika sekta ya mafuta ya Venezuela
Jan 04, 2026 03:02Katika matamshi yake ya uingiliaji kati, Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa Washington itakuwa na nafasi kuu katika sekta ya mafuta ya Venezuela kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya jana ya Marekani dhidi ya Caeacas yaliyopelekea kukamatwa Rais wa Venezuela Nicolas maduro.
-
2025, mwaka wa kushindwa uchumi wa Marekani
Jan 04, 2026 02:40Gazeti la Marekani la Axios limeandika kuwa: Katika mwaka uliomalizika majuzi wa 2025, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa urais wa Donald Trump, uchumi wa Marekani ulifika kwenye ukingo wa mgogoro kutokana na mfumuko wa bei, kupungua kwa ajira, na kutoridhika kwa umma.
-
Afrika Kusini yataka UN iitishe kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Venezuela
Jan 03, 2026 23:31Afrika Kusini imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela, na kukamatwa Rais wa nchi hiyo Nicholas Maduro na mkewe.
-
Nchi mbalimbali zalaani mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela
Jan 03, 2026 23:11Nchi mbalimbali duniani zimeendelea kulaani vikali mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela. Nchi hizo zimeeleza wasiwasi wao kuhusu uhalali, maadili na taathira hatari za uvamizi wa Marekani huko Venezuela.
-
Mkuu wa haki za binadamu wa UN ataka kusitishwa mpango wa Israel wa kuhalalisha kunyongwa Wapalestina
Jan 03, 2026 23:11Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Israel kusitisha mipango yake ya kutoa hukumu za kifo za lazima kwa Wapalestina na kutahadharisha kuwa pendekezo hilo linakiuka sheria za kimataifa.
-
Uhispania: Tuna wasiwasi kuhusu hali mbaya ya Gaza na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi
Jan 03, 2026 23:10Serikali ya Uhispania imeelezea wasiwasi mkubwa ilionao kuhusiana na hali mbaya ya Gaza na muendelezo wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Somalia: Kuitambua Somaliland ni njama za kupotosha walimwengu kuhusu jinai za Israel Gaza
Jan 03, 2026 23:09Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Somalia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hatua ya Israel ya ya kulitambua rasmi eneo la 'Somaliland', ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili kuwa ni njama kupotosha maoni ya umma kutokana na uhalifu unaoendelea kufanywa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
-
Venezuela, mwathirika mpya wa sera inayojikariri ya Marekani
Jan 03, 2026 09:54Tangazo la Rais Nicolás Maduro la kuwa tayari kufanya mazungumzo na Marekani limejibiwa chini ya saa 24 baadaye kwa mashambulizi makali ya kijeshi dhidi ya Caracas, huu ukiwa ni mtindo unaokaririwa wa viongozi wa Washington.
-
Kiongozi Muadhamu: Kwa tawfiq ya Mwenyezi Mungu, tutampigisha magoti adui
Jan 03, 2026 09:02Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu taifa hili litashinda njama zote na kumpigisha magoti adui.