-
Hamas yakataa mpango wa vikosi vya kigeni Gaza
Nov 17, 2025 05:41Makundi ya Kipalestina yakiongozwa na Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Palestina, Hamas, yamepinga vikali mpango wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kupeleka vikosi vya kigeni katika Ukanda wa Gaza.
-
Umoja wa Afrika wakaribisha kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati ya DRC na waasi
Nov 17, 2025 05:39Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, amepongeza kutiwa saini kwa makubaliano ya amanikati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi hayo akisema ni “hatua kubwa kuelekea kurejesha uthabiti, kujenga tena imani, na kushughulikia mizizi ya migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).”
-
Vyombo vya usalama Tanzania vyamkamata raia wa Marekani na Kenya akiwa na mabomu
Nov 17, 2025 00:16Polisi ya Tanzania imetangaza kuwa imemkamata raia wa Marekani na Kenya akiwa na mabomu katika mpaka wa Tanzania na Kenya.
-
Araghchi: Iran lazima ijiimarishe ili kujilinda kwenye ‘Msitu’ ulioundwa na Marekani
Nov 16, 2025 23:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekemea Marekani kwa kuchochea mashindano ya silaha duniani kupitia matumizi ya mabavu waziwazi na uvunjaji wa sheria za kimataifa, akisema hakuna njia nyingine ila kujiimarisha katika “msitu” ulioundwa na Washington.
-
Makundi ya Wapalestina: Hatutaki uwepo wa majeshi ya kigeni Ukanda wa Gaza
Nov 16, 2025 23:36Makundi na harakati za Palestina zimetangaza kuwa zinapinga uwepo wowote wa kijeshi wa kigeni au kambi za kimataifa ndani ya Ukanda wa Gaza, zikisisitiza kwamba suala hilo linawakilisha ukiukwaji wa moja kwa moja mamlaka ya kujitawala ya Wapalestina.
-
Silaha za Australia zinatumika katika mauaji ya kimbari Sudan?
Nov 16, 2025 23:18Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), unaoshutumiwa kwa kuunga mkono waasi wa RSF wanaotekeleza ukatili na mauaji ya kimbari Sudan, umeibuka kuwa soko kubwa zaidi la silaha za Australia.
-
Eslami: Nchi Tatu za Ulaya zinaendeleza mabavu dhidi ya Iran
Nov 16, 2025 23:17Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI), Mohammad Eslami, amesema kuwa Troika ya Ulaya inayojumuisha Ufaransa, Uingereza na Ujerumani inaendeleza mwenendo wa mabavu dhidi ya Iran na imeazimia kuchukua hatua zaidi za uchokozi kuhusu suala la nyuklia la kiraia.
-
Somalia yakaribia uchaguzi wa moja kwa moja, wakazi wa Mogadishu wachukua kadi za kupiga kura
Nov 16, 2025 23:17Somalia imezindua rasmi ugawaji wa kadi za wapiga kura katika mji mkuu, Mogadishu, kuelekea uchaguzi wa manispaa, hatua muhimu katika safari ya taifa hilo kuelekea uchaguzi wa ushiriki wa moja kwa moja wa upigaji kura.
-
Safari inayotia shaka ya ndege kutoka Ghaza, ni mwanzo wa awamu mpya ya kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina?
Nov 16, 2025 22:53Zaidi ya Wapalestina 150 wakazi wa Ukanda wa Ghaza wamehamishwa kwa ndege kutoka eneo hilo la Palestina na kupelekwa Afrika Kusini kwa namna inayotia shaka, huku mamlaka za Afrika Kusini zikieleza kwamba hazikuwa zikijua chochote na kwamba uchunguzi juu ya suala hilo ungali unaendelea.
-
Meja Jenerali Hatami: Hatujawahi kupoteza hata sekunde moja ya kuimarisha nguvu zetu za ulinzi
Nov 16, 2025 07:29Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amesema kuwa, Hatujawahi kupoteza hata sekunde moja katika kuimarisha nguvu za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu na tunajitahidi kwa dhati kuendelea kuboresha nguvu hizo.