-
Gharibabadi: Nchi 3 za Ulaya zimejiondoa zenyewe kwenye diplomasia na Iran
Nov 16, 2025 07:29Naibu Waziri wa Masuala ya Sheria na Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo amesema wakati akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Fars kwamba, Iran itaendelea kuonesha ushirikiano na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kwa mujibu wa hatua zinazochukuliwa na Bodi ya Magavana ya wakala huo na kamwe haitofumbia macho haki yake ya kiimsingi ya kunufaika na teknolojia ya kisasa ya nyuklia.
-
Israel yamuua kigaidi mtaalamu mwingine wa nyuklia wa Misri
Nov 16, 2025 07:28Ingawa maafisa wa Misri wametangaza kwamba wamemkamata mhusika wa mauaji ya mwanasayansi kijana wa nyuklia wa nchi hiyo; lakini taarifa nyingine zinasisitiza kwamba muuaji aliondoka eneo la tukio mbele ya macho ya kila mtu na inaaminika ana uhusiano na shirika la kijasusi la Israel MOSSAD hasa kwa kuzingatia kuwa, Tel Aviv ina historia chafu ya kufanya jinai kama hizo za kuwaua kigaidi wanasayansi wa nyuklia wa nchi mbalimbali ikiwemo Misri.
-
Watu wasiopungua 20 wauawa katika shambulio la waasi wa ADF mashariki mwa DRC
Nov 16, 2025 07:28Kwa uchache watu 20 wamepoteza maisha katika kipindi cha siku mbili za Ijumaa na Jumamosi katika shambulio lililohusishwa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Watu 4 wapoteza maisha baada ya boti za wahamiaji kuzama kwenye pwani ya Libya
Nov 16, 2025 07:27Shiriika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa, kwa uchache watu wanne wamepoteza maisha wakati boti mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji 95 zilipozama kwenye pwani ya mji wa Al Khums wa magharibi mwa Libya.
-
Kutopendelea IAEA upande wowote; takwa kuu la Iran katika kadhia ya nyuklia
Nov 16, 2025 06:54Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuhusu ripoti ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA: "lazima ripoti kama hizo zibaki daima kuwa za kitaalamu, zinazotokana na ukweli halisi, na zisizoathiriwa na utashi wowote wa kisiasa".
-
Pep Guardiola awataka Wahispania kushikamana na Palestina
Nov 16, 2025 03:39Kocha wa Manchester City Mhispania Pep Guardiola, amewataka wananchi wa Uhispania kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina.
-
Rais wa Venezuela: Uadilifu ni sharti la kupatikana amani ya kweli Gaza
Nov 16, 2025 03:38Rais wa Venezuela amesisitiza uungaji mkono kamili kwa haki za watu wa Palestina na haja ya kutekelezwa haki dhidi ya jinai na vitendo vya mauaji ya kimbari.
-
Charlotte Slente: Zaidi ya nusu ya Wasudan wanahitaji msaada wa kibinadamu
Nov 16, 2025 03:37Zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Denmark, huku mapigano yakiliharibu taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika.
-
Walimwengu walaani Wazayuni kuchoma moto msikiti katika Ukingo wa Magharibi
Nov 16, 2025 03:36Hatua ya kundi la walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada ya kuchoma msikiti wa Hajja Hamida katika Ukingo wa Magharibi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu imelaaniwa katika kila kona ya dunia.
-
Hamas yatahadharisha kushadidi janga la kibinadamu Ukanda wa Gaza
Nov 16, 2025 03:35Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeonya kuhusiana na kushadidi janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.