-
Wasudan 177,000 wamekwama katika mji ulioteketea
Nov 02, 2025 22:53Mji wa El Fasher, ambao ni makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, hatimaye ulitekwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF hivi karibuni baada ya kuzingirwa kwa muda wa miezi 18 na hivi sasa ripoti zinasema kuwa Wasudan 177,000 wamekwama kwenye mji huo.
-
Marekani haina uwezo wa kukabiliana na kombora la Burevestnik la Russia
Nov 02, 2025 22:52Afisa wa zamani wa masuala ya kijasusi wa Marekani ambaye pia ni mkaguzi wa zamani wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba Marekani haina mfumo wa ulinzi wa makombora unaoweza kukabiliana na shambulio la kombora la Burevestnik la Russia.
-
Wahamiaji 45 wasio na vibali waokolewa pwani ya mashariki ya Libya
Nov 02, 2025 22:51Wahamiaji 45 wasio na vibali wameokolewa kwenye pwani ya mji wa Tobruk wa mashariki mwa Libya. Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Libya Al-Watan ambalo limesema kuwa wahamiaji hao wamekabidhiwa kwa mamlaka husika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
-
Rais Pezeshkian: Sekta ya nyuklia ya Iran inalenga ustawi wa umma, si silaha za nyuklia
Nov 02, 2025 08:29Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kwamba ustawi wa sekta yake ya nyuklia ya amani nchini Iran unalenga kuimarisha ustawi wa taifa, si kupata silaha.
-
Kuna taathira gani za kufukuzwa Mwanamfalme Andrew katika mfumo wa ufalme wa Uingereza?
Nov 02, 2025 08:04Mapema usiku wa Ijumaa, Kasri ya Buckingham ilitoa taarifa rasmi ikitangaza kwamba Mwanamfalme Andrew amevuliwa vyeo vyote vya kifalme, majukumu rasmi na fursa za heshima, uamuzi ambao Mfalme Charles III aliutaja kuwa "usioepukika" kwa ajili ya kuepusha taasisi ya ufalme kuzama kwenye wimbi la kutoaminika nchini Uingereza.
-
Umoja wa Afrika wampongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania
Nov 02, 2025 07:58Umoja wa Afrika umempongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuingoza Tanazania kwa muhula mwigine baada ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29 mwezi uliopita wa Oktoba.
-
Obama: Nyakati za giza zinatawala Marekani
Nov 02, 2025 07:39Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amemkosoa vikali Donald Trump, akiutaja utawala wake kuwa ni "kielelezo cha uasi na mparaganyiko" na kuwashutumu Warepublican kwa kukaa kimya mbele ya mienendo yake ya kutowajibika.
-
Rais Pezeshkian aipongeza Algeria kwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru
Nov 02, 2025 07:14Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa pongezi za dhati kwa Rais na watu wa Algeria kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 71 ya kuanza Mapinduzi ya Ukombozi na Siku ya Taifa ya Algeria na kusema: Uhusiano wa kihistoria kati ya Iran na Algeria unafungua njia ya kupanuliwa zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
-
Nigeria yapinga vikali vitisho vya Trump, yasema mamlaka yake ya kujitawala hayajadiliwi
Nov 02, 2025 07:11Serikali ya Nigeria imepinga vikali uingiliaji wowote wa kigeni katika mambo ya ndani ya nchi hiyo ikisisitiza kwamba "mamlaka ya kitaifa hayawezi kujadiliwa," na kwamba inachunguza matukio ya hivi karibuni na kuwafuatilia wale wote waliohusika.
-
Israel yaendelea kuwatesa kwa njaa Wapalestina kwa kuruhusu 24% tu ya misaada kuingizwa Ghaza
Nov 02, 2025 03:20Mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimetangaza kuwa utawala wa kizayuni wa Israel umeruhusu kuingizwa katika eneo hilo sehemu ndogo tu ya misaada ya kibinadamu kinyume na ilivyoafikiwa katika makubaliano ya usitishaji mapigano yanayosimamiwa na serikali ya Marekani, ambayo yalianza kutekelezwa mwezi uliopita.