-
Watanzania leo wanamchagua Rais, Wabunge na madiwani
Oct 28, 2025 23:32Watanzania waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais, Wabunge na madiwani katika uchaguzi uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA.
-
Upeo mpya katika mahusiano ya kibiashara wa Iran na Pakistan; biashara ya kubadilishana, hatua mpya ya kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi
Oct 28, 2025 22:56Matukio chanya yametokea katika wiki za hivi karibuni katika suala la kuongeza uhusiano wa kibiashara na mawasiliano kati ya Iran na Pakistan.
-
'Ni Hatari': Iran yalaani uchochezi wa kijeshi wa Marekani huko Venezuela
Oct 28, 2025 14:26Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani uchochezi wa kijeshi wa Marekani kandokando ya Venezuela ikisema ni tishio kwa amani na usalama katika eneo la Karibi na Amerika Kusini.
-
Majibu makali ya mwandishi Msaudia kwa waziri wa Israel: Ngamia wetu wana asili, nyinyi hamnayo
Oct 28, 2025 14:26Mwandishi wa Saudi Arabia na mchambuzi wa masuala ya kisiasa amejibu matamshi ya dharau yaliyotolewa na Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich akisema, "Ngamia wetu wana asili, lakini nyingi hamna asili."
-
UNRWA: Msimamo wa Marekani hautatuzuia kufanya kazi yetu huko Gaza
Oct 28, 2025 14:25Adnan Abu Hasna, mshauri wa vyombo vya habari wa Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Palestina (UNRWA), amesema kwamba taarifa za hivi karibuni za Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambapo alidai shirika hilo la kimataifa halitakuwa na nafasi yoyote katika Ukanda wa Gaza, si jambo jipya na ni katika fremu ya misimamo ya Marekani kuhusu taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Senegal yachunguza mauaji ya kikoloni ya Ufaransa baada ya uchimbaji mpya, Thiaroye
Oct 28, 2025 14:25Wanaakiolojia nchini Senegal wamegundua ushahidi mpya wa mauaji ya kikoloni ya Ufaransa yaliyotokea mwaka 1944, kama sehemu ya juhudi zinazoongozwa na serikali za kufichua ukweli kuhusu mauaji yaliyofanywa na vikosi vya jeshi la Ufaransa baada ya Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya ya wanajeshi wa Afrika Magharibi.
-
Mshauri wa kijeshi wa Ayatullah Khamenei: Iran iko tayari kwa 'vita vya korido' ili kuongeza ushawishi wa kimkakati
Oct 28, 2025 08:53Mshauri mkuu wa kijeshi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametaja "vita vya korido" vinavyoibuka kuwa ni uwanja muhimu katika uhusiano wa kimataifa, na uwanja mpya wa ushawishi wa kimkakati wa Iran.
-
Mgogoro wa El Fasher: Maelfu wakadiriwa kuuawa, Umoja wa Afrika walaani "ukatili"
Oct 28, 2025 08:52Waziri wa Afya katika jimbo la Darfur, Babiker Hamdeen amesema kwamba maelfu ya raia wameuawa katika mji wa El Fasher katika siku mbili zilizopita, huku Umoja wa Afrika ukilaani "ukatili" na "madai ya kufanyika uhalifu wa kivita" huko El Fasher, magharibi mwa Sudan.
-
Maandamano ya Tunisia na Morocco; dhihirisho la kuunga mkono Wapalestina barani Afrika
Oct 28, 2025 08:15Wimbi jipya la uungaji mkono kwa Wapalestina barani Afrika limekwenda sambamba na kulaani vitendo vya kijinai vya utawala haramu wa Israel.
-
Ajali ya ndege yaua 12 Kenya wakiwemo watalii wa kigeni
Oct 28, 2025 08:02Watu 12, wakiwemo watalii, wanahofiwa kufariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea katika eneo la Vyungwani, Matuga, Kaunti ya Kwale, mapema leo Jumanne.