-
Pezeshkian atoa wito wa kubuniwa mfumo wa usalama' wenye msikamano ndani ya kambi ya ECO
Oct 28, 2025 07:25Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya ECO kuanzisha na kutekeleza mfumo thabiti wa usalama, unaounda utulivu, wa ndani, na unaozingatia maendeleo.
-
Watu wenye hasira waendelea kuandamana Cameroon kupinga ushindi wa Paul Biya
Oct 28, 2025 05:42Maeneo mbalimbali ya Cameroon yameendelea kushuhhudia maandamano ya watu wenye hasira wanaopinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais kizee zaidi duniani yaani Paul Biya mwenye umri wa miaka 92.
-
OHCHR: Waasi wa RSF wamefanya ukatili wa kutisha nchini Sudan
Oct 28, 2025 04:26Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema imepokea taarifa za kutisha kuwa waasi wa RSF wanafanya ukatili wa kutisha nchini Sudan.
-
Maduro: Marekani inalenga kupora mafuta, gesi na dhahabu ya Venezuela
Oct 28, 2025 04:25Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, amesisitiza kuwa ulimwengu mzima unafahamu kuwa mabepari wanaotawala Marekani wanataka kupora mafuta, gesi na dhahabu ya nchi yake.
-
Uchaguzi wa mapema unafanyika Zanzibar leo
Oct 28, 2025 04:23Leo, visiwa vya Zanzibar vimeingia katika hatua muhimu ya mchakato wa uchaguzi kwa kuanza rasmi zoezi la kupiga kura ya mapema, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 29, katika Tanzania Bara na visiwani.
-
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara ashinda kwa kishindo muhula wa nne wa urais
Oct 28, 2025 04:22Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka huu, akijihakikishia muhula wa nne madarakani kwa ushindi mkubwa wa asilimia 89.77% ya kura zote.
-
Iran kuvutia watalii Waislamu wanaotaka huduma 'Halal'
Oct 28, 2025 04:21Waziri wa Urithi wa Kitamaduni, Utalii na Sanaa za Mikono wa Iran, Seyyed Reza Salehi Amiri, amesema kuwa utalii 'Halal' ni jukwaa muhimu katika kukuza mwingiliano wa kitamaduni na kuwavutia wageni Waislamu.
-
Makubaliano ya mpaka kati ya Iran na Afghanistan
Oct 28, 2025 02:25Kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa mpaka kati ya Iran na Afghanistan kimefanyika kwa kuhudhuriwa ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.
-
Idadi ya mashahidi huko Gaza imefikia 68,527
Oct 28, 2025 02:21Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza imefikia 68,527.
-
Pezeshkian: Iran na Oman zimekuwa wasaidizi wa kila mmoja katika misukosuko ya kikanda
Oct 27, 2025 23:46Rais Masoud Pezeshkian amesisitiza historia ya muda mrefu na yenye upendo ya uhusiano kati ya Iran na Oman na kusema: "Mawasiliano na maingiliano kati yao yamekuwa yakiegemezwa katika misingi ya udugu, kuheshimiana na nia njema, na nchi hizo mbili daima zimekuwa ni wasaidizi na waungaji mkono wa kila mmoja katika hali ya misukosuko ya kieneo."