-
UNHCR yaonya juu ya ukandamizaji wa haki za wakimbizi
Jul 30, 2026 04:04Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema haki za waomba hifadhi ulimwenguni zinakabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa. Hayo yameelezwa wakati shirika hilo likiadhimisha miaka 75 ya kupitishwa kwa Mkataba wa Wakimbiuzi.
-
Zakharova: Shambulio la Ukraine dhidi ya meli ya Iran lilikuwa kitendo cha wazi cha ugaidi
Jul 30, 2026 04:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameikosoa vikali serikali ya Kyiv, akisisitiza kuwa shambulio la Ukraine dhidi ya meli ya Iran lilikuwa mfano halisi wa kitendo cha kigaidi.
-
Mgogoro katika Jeshi la Israel: Wanajeshi wengine wawili wa Kizayuni wajiua
Jul 30, 2026 04:00Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimeripoti kuwa, baada ya wanajeshi wengine wawili wa Kizayuni kujiua, idadi ya wanajeshi waliojitoa uhai tangu mwanzoni mwa mwaka huu imefikia 16.
-
Jeshi la Iran lashambulia kambi ya anga ya Marekani Jordan, lasimamisha meli Hormuz
Jul 29, 2026 14:33Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetekeleza shambulizi la kulipiza kisasi kwa makombora ya balistiki dhidi ya kambi ya Jeshi la Anga la Marekani nchini Jordan, sambamba na kusimamisha meli tatu zilizoingia kinyume cha sheria katika Lango Bahari la Hormuz.
-
Iran yaonya: Hujuma za Marekani na Israsel ni tishio kwa amani duniani
Jul 29, 2026 14:28Iran imeonya kuwa kuendelea kwa hujuma za kijeshi za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza, mashambulizi dhidi ya nchi jirani, na upanuzi wa makazi haramu, sambamba na hujuma zisizo halali za Marekani dhidi ya Iran, kunaleta tishio kubwa kwa amani ya kikanda na ya kimataifa huku ikisisitiza tena haki yake ya kujilinda.
-
Taasisi ya Royan ya Iran ni miongoni mwa taasisi 10 bora duniani katika kutibu ugumba
Jul 29, 2026 14:25Taasisi ya Utafiti ya Royan ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetajwa kuwa miongoni mwa taasisi kumi zenye ushawishi mkubwa zaidi duniani katika masuala ya utafiti wa ugumba wa kiume na teknolojia ya usaidizi wa uzazi (ART) ikishika nafasi ya tisa kimataifa.
-
Rais wa Algeria akemea ‘serikali ndogo’ ya kikanda kwa uvurugaji usalama, akusudia UAE
Jul 29, 2026 14:19Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, ameikosoa vikali “serikali ndogo” ya kikanda ambayo hakuitaja jina, lakini inafahamika wazi kuwa alikusudia Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kutokana na mchango wake wa kuvuruga usalama na utulivu katika ulimwengu wa Kiarabu na ukanda wa Sahel eneo la Afrika Magharibi, akionya kuwa Algeria itasimama imara kulinda mamlaka yake.
-
Uganda yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa homa ya Ebola nchini humo
Jul 29, 2026 14:16Mamlaka nchini Uganda zimetangaza kuwa nchi hiyo sasa haina maambukizi ya virusi vya Ebola, huku maambukizi ya ugonjwa huo wa homa ya kutokwa damu yakiendelea kuongezeka katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Ripoti: Iran inadhihirisha uwezo unaoongezeka wa kushambulia shabaha za kijeshi za US kupitia operesheni za pamoja
Jul 29, 2026 02:59Iran imeonyesha uwezo unaoongezeka wa kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani kote Asia Magharibi kwa kuchanganya ndege zisizo na rubani za mashambulizi na makombora ya kisasa ya balestiki. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyomnukuu ripoti afisa wa ngazi ya juu wa Marekani.
-
'Nchi yoyote inayopokea pesa kutoka kwenye mali za Iran hairuhusiwi kupita katika Mlango-Bahari wa Hormuz'
Jul 29, 2026 02:41Msemaji wa Makao Makuu ya Kijeshi ya Khatamul-Anbiyaa amesema: "Kampuni au nchi yoyote ile itakayopokea pesa kutoka kwenye mali za Iran haitaruhusiwa kupita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz."