-
Qalibaf: Mpangilio mpya wa Kiislamu uundwe baada ya Marekani na Israel kudhalilishwa katika vita dhidi ya Iran
Jun 25, 2026 04:27Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa wito kwa mataifa ya Asia Magharibi na ulimwengu wa Kiislamu kuanzisha mpangilio mpya wa kikanda unaotegemea uwezo, rasilimali na watu wa mataifa hayo, akisisitiza kwamba “chanzo cha misiba yote ni utawala wa Kizayuni.”
-
Hizbullah: Israel haiwezi kamwe kufikia malengo yake katika medani ya vita
Jun 25, 2026 04:25Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, ameashiria "kugonga mwamba wa mradi wa Israel," na kusisitiza kwamba, utawala huu hautaweza kamwe kufikia malengo yake katika medani ya vita.
-
Iran yapendekeza kuanzishwa Umoja wa Redio na Televisheni wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai
Jun 25, 2026 04:22Mwakilishi wa Mkuu wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ametoa pendekezo la kuanzishwa Umoja wa Redio na Televisheni wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai kama utaratibu mpya wa kuimarisha diplomasia ya vyombo vya habari na muungano wa kitamaduni miongoni mwa nchi wanachama.
-
Umoja wa Mataifa: Watoto milioni 100 wameachishwa shule kutokana na migogoro
Jun 25, 2026 04:18Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watoto milioni 100 wameachishwa shule kutokana na migogoro.
-
WHO: Hakuna hospitali yoyote Gaza inayofanya kazi kwa uwezo wake kamili
Jun 25, 2026 04:14Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba hakuna hospitali yoyote katika Ukanda wa Gaza inayofanya kazi kwa uwezo wake kamili kwa sasa, na kwamba, uhaba mkubwa wa vifaa vya matibabu na mafuta umeweka utoaji wa huduma za afya katika hatari kubwa.
-
Mamilioni ya Wairani washiriki maombolezo kuelekea siku ya Ashura
Jun 24, 2026 11:04Mamilioni ya Waislamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maeneo mengine ya dunia leo mchana wameshiriki katika maombolezo ya kumbukumbu ya Ta'asua na jioni hii wanashiriki katika hafla za mkesha wa Ashura ambayo ni kukumbuka siku ya kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS).
-
Qalibaf: Mkataba wa Islamabad ni tangazo la kufeli kwa Marekani
Jun 24, 2026 11:00Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Mkataba wa Maelewano (MoU) wa kumaliza vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran haukuwa matokeo ya shinikizo au kulazimishwa, bali ni zao la ustahimilivu na nguvu ya taifa shupavu la Iran.
-
Pezeshkian: Iran haitazungumzia uwezo wake wa kjeshi, asema makombora yameiepusha Iran na hatima ya Gaza
Jun 24, 2026 10:59Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa Tehran haitawahi kamwe kufanya mazungumzo yoyote kuhusu uwezo wake wa ulinzi na kuzuia uchokozi (deterrence), akibainisha kuwa ghala la makombora la nchi hii ndilo limeiweka Iran salama dhidi ya kukumbwa na hatima ya Gaza.
-
Watafiti wa Iran wapiga hatua ya kwanza katika chanjo ya mRNA dhidi ya saratani ya matiti
Jun 24, 2026 10:57Watafiti kutoka taasisi tano za kisayansi na kitiba nchini Iran wamefanikiwa kubuni chanjo ya aina yake ya mRNA kwa kutumia njia za hali ya juu za kompyuta.
-
Kenya yaisitisha ujenzi wa kituo cha Ebola cha Marekani
Jun 24, 2026 10:51Wizara ya Afya ya Kenya imesitisha ujenzi wa kituo cha karantini cha ugonjwa wa Ebola kinachozua utata, ambacho kinamilikiwa na Marekani, baada ya changamoto ya kisheria kuhoji uhalali wa mradi huo na hatari zake kwa jamii.