-
Hatua ya Israel ya kubomoa makao makuu ya UNRWA yaendelea kulaaniwa kimataifa
Jan 29, 2026 00:16Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tisa za Ulaya, pamoja na Kanada na Japan, wamelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kubomoa makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
-
Mdororo wa uchumi US; UPS kuwafuta kazi watu 30,000
Jan 28, 2026 23:54Kampuni ya kusafirisha mizigo ya United Parcel Service (UPS) ya Marekani imetangaza kwamba, itawatimua kazi watu 30,000 zaidi mwaka huu, katika juhudi za kupunguza ushirikiano wake na shirika la Amazon, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mpango wake wa 'uokoaji' na kubana matumizi.
-
Je, Tel Aviv inalenga kuizingira kimkakati Misri katika Bahari Nyekundu?
Jan 28, 2026 23:54Misri, katika kujibu kuongezeka kwa ushawishi na uingiliaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Pembe ya Afrika, imeimarisha uwepo wake wa kijeshi nchini Somalia.
-
Jeshi la Niger lasema zaidi ya magaidi 70 "wameangamizwa"
Jan 28, 2026 09:49Jeshi la Niger limesema kwamba, zaidi ya magaidi 70 "waliangamizwa" kote nchini kati ya Januari 19 na 25, wakiwemo zaidi ya 50 waliouawa katika mashambulizi ya anga yaliyolenga "mikusanyiko ya maadui."
-
HAMAS: Hakuna suala la upokonyaji silaha madamu uvamizi na ukaliaji wa ardhi unaendelea
Jan 28, 2026 07:35Afisa mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, amejibu vitisho vilivyotolewa na waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel kuhusu upokonyaji silaha huko Ghaza na kusisitiza kwamba, silaha za Muqawama zinahusiana na mwendelezo wa uvamizi na kukaliwa ardhi za Palestina kwa mabavu, na kwamba huo ni uamuzi wa kitaifa ambao hautaachwa hadi uvamizi utakapokomeshwa.
-
Mtaalamu wa kijeshi: Utitiri wa droni za Iran ni 'tishio halisi' kwa vyombo vya majini vya Marekani
Jan 28, 2026 07:02Mtaalamu wa kijeshi wa ndege zisizo na rubani ameonya kuwa, utitiri wa ndege zisizo na rubani za Iran ni "tishio halisi" kwa vyombo vya jeshi la wanamaji la Marekani vyenye thamani kubwa, wakati huu ambapo Washington inaripotiwa kuwa inaendelea kujizatiti kijeshi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Trump atishia kuikatia misaada Iraq endapo Nouri al-Maliki atakuwa Waziri Mkuu
Jan 28, 2026 06:58Rais wa Marekani Donald Trump amedai katika ujumbe unaoakisi uingiliaji wa wazi wa masuala ya ndani ya Iraq kwamba Nouri al-Maliki hapasi kuwa waziri mkuu, kwa sababu kama atachaguliwa kushika wadhifa huo, Marekani haitatoa tena misaada kwa nchi hiyo.
-
Yemen yatoa onyo la kuishambulia manowari ya Marekani ikikiuka mzingiro wa Bahari Nyekundu
Jan 28, 2026 06:50Harakati ya Ansarullah ya Yemen, leo imetoa indhari kwa kukumbusha shambulio lake la huko ililofanya kwa mafanikio dhidi ya meli ya mafuta ya Uingereza ya "Marlin Luanda" katika Ghuba ya Aden kufuatia ukiukaji wa mzingiro wa majini uliowekwa na harakati hiyo dhidi ya Israel,
-
Rais wa Ukraine aliagiza jeshi liue 'makumi ya maelfu ya Warusi'
Jan 28, 2026 06:49Jeshi la Ukraine linapaswa lijikite katika kusababisha vifo vingi zaidi kwa Russia kadiri iwezekanavyo. Hayo yametamkwa na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky na kusisitiza kwamba, idadi ya vifo 50,000 vya Warusi kwa mwezi ni "kiwango bora" ambacho wanajeshi wa Ukraine wanapaswa wajitahidi kukifikia.
-
Iran ilivyofanikiwa kuvunja mtandao wa mawasiliano ya kigaidi kwa kukata intaneti
Jan 28, 2026 04:30Iran ilifanikiwa kuvuruga na hatimaye kuvunja mtandao wa mawasiliano wa makundi ya kigaidi na washirika wao wa nje kwa hatua ya kukata intaneti wakati wa machafuko ya Januari 2026.