Oct 04, 2023 06:48 UTC
  • Al Sudani: Iraq inapinga kukiukwa mamlaka ya kujitawala ya nchi jirani

Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba nchi yake haitageuzwa kuwa sehemu ya kukika mamlaka ya kujitawala ya nchi yoyote ile hasa nchi jirani.

Mohammed Shia al Sudani ameeleza kuwa, nchi yake haitakiuka mamlala ya kujitawala ya nchi nyingine na kwamba Baghdad haitaruhusu kutumiwa ardhi ya Iraq kutekeleza mashambulizi dhidi ya nchi nyingine hususan nchi jirani. 

Al Sudani ameongeza kuwa: "Tunawanyooshea mikono ndugu na marafiki wote kwa ajili ya kuanzisha uhusiano mwema na majirani zetu."  

Mohammed Shia al Sudan amesema: Tuna uwezo wa kulinda ardhi ya Iraq na kulinda mamlala ya kujitawala na hii ni dhamira ya kitaifa ya kuwajibika ambayo hatutaikengeuka.  

Waziri Mkuu wa Iraq amesema, katika serikali ya sasa ambayo inakaribia mwishoni mwa mwaka wake wa kwanza tunaamini katika  uhusiano wa nje na mataifa mbalimbali kwa mujibu wa maslahi yetu ya taifa.    

Tags