Oct 14, 2023 03:28 UTC
  • Abdollahian na Nasrullah wazungumzia matukio ya karibuni kuhusu vita vya Gaza

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Sayyed Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah Sayyed katika ziara yake nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iranpress, katika mazungumzo hayo, Hussein Amir-Abdollahian Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran alishauriana na Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi hususan mashambulizi ya kushtukiza ya Harakati ya Muqawama ya Hamas katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni kuendelea Israel kuwashambulia raia wasio na hatia huko Gaza.

Amir-Abdollahian akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Iran aliondoka Baghdad na kuwasili Beirut siku ya  Alkhamisi ambapo mbali na kukutana na Katibu Mkuu wa Hizbullah jana alikutana na kufanya mazungumzo pia  na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati.

Hussein Amir Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akiwa katika mazungumzo na Najib Mikati, Waziri Mkuu wa Lebanon

 

Katika muendelezo wa mashauriano yake na viongozi mbalimbali wa Lebanon, Abdollahian amekutana na kufanya mazungumzo pia na Spika wa Bunge na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo.

Imeelezwa kuwa, kuchunguzwa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza ndio lengo kuu la mashauriano ya Amir Abdollahian na viongozi wa Iraq na Lebanon. Katika mashauriano hayo, pande hizo zimejadili masuala kadhaa na kueleza mtazamo mmoja kuhusu vita dhidi ya Gaza.

Tags