Nov 13, 2023 14:41 UTC

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kutekeleza mauaji ya kimbari huko Gaza Palestina huku asasi zote muhimu za kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zikishindwa kusitisha unyama huo wa Israel.

Katika upande mwingine, watu huru na wapigania haki wameendelea kufanya maandamano katika maeneo tofauto duniani kulaani jinai hizo. Salum Bendera amezungumza na Sheikh Stambuli Abdillah Nassir, msomi, mwanahistoria na mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla wa Mombasa Kenya ambaye kwa kuanzia anaelezea tathmini yake kuhusiana na kile kinachojiri hivi sasa huko Gaza. 

Hii ikiwa ni sehemu ya kwanza.