Feb 25, 2024 02:39 UTC
  • Askari wasiopungua sita za Kizayuni waangamizwa na Wanamuqawama wa Palestina Khan Yunis

Brigedi za Mujahidina wa Palestina zimetangaza kuwa zimewaangamiza wanajeshi kadhaa wa Kizayuni katika operesheni ya karibuni zaidi iliyotekelezwa na Muqawama wa Palestina magharibi mwa Khan Yunis.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, brigedi za Mujahidina wa Palestina zimeeleza katika taarifa kwamba, zimefanya operesheni ya mashambulio kwa kushirikiana na vikosi vya Quds (tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina) ambapo askari sita wa Kizayuni waliangamizwa na wadunguzi wa Kipalestina. Waliangamia.
 
Brigedi za Al-Aqsa nazo pia zimetangaza katika taarifa kwamba: vituo vya mkusanyiko wa wanajeshi wa Kizayuni katika eneo la Netsarim kaskazini mashariki vimeshambuliwa kwa maroketi 107.

Taarifa ya Brigedi za Al-Aqsa imeeleza pia kwamba ngome za Wazayuni katika mji wa Khan Yunis zimeshambuliwa kwa maguruneti ya wanamuqawama.

Mujahidina wa Harakati ya Jihadul-Islami

Wakati huo huo vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kujiri kwa tukio kubwa la kiusalama huko kusini mwa Ghazza na kutangaza kuwa askari wasiopungua saba wa utawala huo wameuawa.

Ikumbukwe kuwa, tangu tarehe 7 Oktoba 2023 na kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji makubwa na ya kinyama katika Ukanda wa Ghazza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina, na kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu mbele ya jinai za Israel zimepelekea kuendelezwa mauaji hayo yanayowalenga zaidi wanawake na watoto wa Kipalestina.../

Tags